Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dodoma Jiji yashtukia janja ya Azam FC

KIPWAGILE Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo wa zamani wa Polisi Tanzania, KMC FC na Namungo FC, ameonyesha kiwango kizuri msimu huu na kuanza kuzivutia timu mbalimbali zilizokuwa zinahitaji saini yake, ikiwemo matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC aliyowahi kuichezea.

BAADA ya Azam FC kumpigia hesabu za kumrejesha aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa kikosi hicho, Idd Kipagwile, mabosi wa Dodoma Jiji wameshtukia dili hilo mapema na kuamua kumwongezea mkataba wa miaka miwili baada ya huu wa sasa kumalizika.

Nyota huyo wa zamani wa Polisi Tanzania, KMC FC na Namungo FC, ameonyesha kiwango kizuri msimu huu na kuanza kuzivutia timu mbalimbali zilizokuwa zinahitaji saini yake, ikiwemo matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC aliyowahi kuichezea.

Akizungumza na Mwanaspoti, Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fortunatus Johnson alisema wamemwongezea mkataba wa miaka miwili nyota huyo wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho, huku wakiendelea na mazungumzo na wengine ambao wamemaliza msimu huu.

“Mbali na Kipagwile ila tumemuongezea pia mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wetu, Yassin Mgaza na tunaendelea na wale ambao wamemaliza, nafikiria kuanzia Julai 10, 2025, tutakuwa tumefikia sehemu nzuri zaidi ya sasa,” alisema Fortunatus.

Msimu huu wa 2024-2025, Kipagwile amechangia mabao 11 ya Ligi Kuu Bara kati ya 31, yaliyofungwa na Dodoma Jiji, baada ya kufunga saba na kuasisti mengine manne na amekiwezesha kikosi hicho kumaliza kikiwa nafasi ya 12 na pointi zake 34.

Kipagwile amemaliza nafasi ya pili kwa kufunga mabao mengi zaidi katika kikosi cha Dodoma Jiji, akizidiwa na Paul Peter aliyeondoka baada ya mkataba wake kuisha aliyefunga manane na kuasisti mawili.