Djuma azua hofu Yanga
BEKI Djuma Shaban wa Yanga baada ya kurejea amejikuta akizua hofu kutokana na kushindwa kumaliza mazoezi yanayoendelea katika uwanja wa Highland, Morogoro.
Djuma alikosekana kwenye mechi za awali baada ya kufungiwa mechi tatu na Bodi ya Ligi Kuu Bara
Mchezaji huyo alianza vizuri mazoezi na wenzake na kufanya kila zoezi ambalo lilikuwa linatolewa uwanjani hapa .
Kocha Nasreddine Nabi baada ya kumaliza mazoezi mepesi alipanga vikosi viwili akianza na Diara Djigui, Djuma Shaban, Farid Mussa, Yanick Bangala na Bakari Mwamnyeto.
Khalid Aucho, Dickson Ambundo, Salum Abubakar, Fiston Mayele, Mapinduzi Balama na Saido Ntibazonkiza.
Kikosi kingine kikiwa na Eric Johora, Kibwana Shomari (Alicheza kama beki wa kulia), Yassin Mustapha, Zawadi Mauya, Ibrahim Ahmad, Feisal Salum,Yusuph Athuman, Deus Kaseke, Heritier Makambo na Denis Nkane.
Mchezaji huyo alionekana kuwa na ufiti wa kucheza lakini mazoezi yakiwa yanaendelea alizua hofu baada ya kushindwa kumaliza mazoezi akikaa chini na nafasi yake alienda kucheza Paul Godfrey 'Boxer'.