Diarra: Haijaisha hadi iishe

GOLIKIPA wa Yanga, Djigui Diarra amesema wameshindwa vita ya fainali ya mchezo wa kwanza uliopigwa katika Uwanja wa Mkapa lakini watapambana kwa nguvu zote kurudi upya kwa ushindi.
Wikiendi iliyopita Yanga ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa USM Alger ikiwa nyumbani na kichapo hiko kuwafanya wananchi kuwa na mzigo mkubwa wa kushinda ugenini.
Diarra ameandika maneno hayo katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuongeza kuwa kushindwa kwao vita bado haijaisha mpaka pale ambapo wanamaliza dakika 90 nyingine katika mechi ya marudiano Juni 3 nchini Algeria.
"Fainali ya CAF inachezwa katika dakika 180 kamili tulishindwa mapigano lakini sio vita, tutarudi kwa nguvu zaidi na kwa pamoja tutaandika historia," alisema Diarra