Dakika 120 zashindwa kutoa bingwa wa ASFC

Dakika 120 zimekamilika katika mchezo wa Ligi ya Kombe la Shirikisho bila Yanga Wala Coastal kuwa na uhakika wa kubeba ndoo baada ya kutoka sare ya 3-3.
Mchezo huo unaopigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, umemalizika dakika 120 baada ya 90 za awali kukamilika bila kupatikana bingwa huku ikisubiriwa hatua ya penalti.
Coastal iliianza kupata bao dakika ya 10 kupitia Abdul Sopu ambaye aliunganisha krosi ya Vicent Aboubakar.
Kipindi Cha pili dakika ya 57 Feisal Salum alifanikiwa kuisawazishia timu yake bao hilo kabla ya dakika ya 84 Heritier Makambo kuwanyanyua mashabiki kwa bao la pili.
Mashabiki wa Yanga wakiwa na uhakika wa kubeba ndoo kwa nyimbo mbali mbali za furaha huku wakiitaja GSM na wengine wakionyesha ishara ya kuchinja ghafla walinyamazishwa na bao la kusawazisha la Sopu dakika ya 86.
Utulivu zaidi ulitawala kwa mashabiki wa pande zote katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya filimbi ya mwamuzi Ahmed Arajiga kutoka Arusha kupulizwa kuashiria Dakika 120 kumalizika.
Katika dakika 30 za nyongeza Sopu aliifungia timu yake bao ya tatu Dakika ya 104 kabla ya Denis Nkane kuisawazishia Yanga dakika ya 118.
Kwa Sasa kinachosubiriwa na hatua ya matuta kuamua nani bingwa kati ya Yanga au Coastal union.