Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coutinho, Tegete ndiyo basi tena Yanga

Muktasari:

  • Lakini benchi la ufundi la Yanga limewatoa hofu mashabiki na kusisitiza kwamba nafasi ya Coutinho itachezwa na Mrisho Ngassa ambaye yupo katika ubora wake.

UWEZEKANO wa Andrey Coutinho wa Yanga kucheza mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Azam keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam  ni finyu. Si yeye tu hata straika, Jerry Tegete, anahisi maumivu na amekiri hatakuwa fiti kwa mchezo huo.

Lakini benchi la ufundi la Yanga limewatoa hofu mashabiki na kusisitiza kwamba nafasi ya Coutinho itachezwa na Mrisho Ngassa ambaye yupo katika ubora wake.

Katika mazoezi ya jana Alhamisi, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kiungo  Coutinho na Tegete hawakufanya na kwa mujibu wa Daktari wa Yanga, Juma Sufiani, Coutinho anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu, Cannavaro anaumwa nyama za paja na Tegete anasumbuliwa na nyonga.

“Coutinho anasumbuliwa na enka na uhakika kama atacheza mechi na Azam au vipi nadhani hadi kesho (leo Ijumaa) jioni nitajua mambo yanaendaje kwani natakiwa kumtazama kwa karibu mno.

“Kwa Tegete na Cannavaro wao wana maumivu madogo na kesho (leo) wanaweza kufanya mazoezi halafu kocha ndiye atakayeamua kama watafaa kucheza na Azam au vinginevyo,” alisema Sufiani.

Hata hivyo, Mwanaspoti lilifanya mahojiano na Tegete kuhusu hali yake ambapo alisema: “Naumwa nyonga na zimenibana sana, sitacheza mechi ya Azam kwani hata kama nikijisikia vizuri muda utakuwa mdogo wa kujiandaa.”

Tegete alifika katika mazoezi ya Yanga Uwanja wa Sekondari ya Loyola lakini aliondoka kabla ya kumalizika kwa mazoezi hayo.

Jana jioni kikosi cha Yanga kiliingia kambini Bagamoyo kujiandaa na mechi hiyo inayoashiria ufunguzi wa msimu mpya.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva, amesem: “Ngassa ana kasi nzuri, ana mbinu na ni mjanja anapokuwa na mpira, naamini ni mbadala tosha wa Coutinho.

“Kingine ambacho kinatupa furaha kuhusu Ngassa kuelekea mchezo wa Ngao ya hisani dhidi ya Azam ni kuwa Ngassa ana uwezo mkubwa wa kufunga magoli.”

Ngassa alianza mazoezi jana asubuhi baada ya awali kuripotiwa kuwa kiungo huyo mshambuliaji aligoma kushinikiza maslahi yake.

Wachezaji ambao waliunda kikosi hicho na wataweza kucheza jumapili dhidi ya Azam ni Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga pamoja na Genilson Santos ‘Jaja’.