Chuo cha NIT chawataka wafanyakazi wake kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi

Monday June 21 2021
New Content Item (1)

Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakicheza mchezo wa kuvuta kamba

CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimewataka wafanyakazi wake kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mbalimbali yakiwemo ya viungo kwa lengo la kutunza afya zao.

Hayo yamebainishwa na Naibu Mkuu wa Chuo hicho cha Taifa cha Usafirishaji, Profesa Prosper Mgaya, wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzunduzi wa bonanza kwa watumishi wote wa chuo lililofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho eneo la Mabibo Mkoani Dar es Salaam ikiwa sehemu ya maadhimisbo ya wiki ya utumishi wa umma.

Profesa Mgaya amesema kuwa wameona kuadhimisha wiki hiyo kwa vitendo kwa kufanya bonanza la michezo ambalo linalengo la kuwakumbusha wafanyakazi juu ya umuhimu wa ufanyaji wa mazoezi.

“Lengo la bonanza hili la Michezo ni kuwaonesha wafanyakazi wetu kuwa ni muhimu kufanya mazoezi ili kuweka afya yako katika hali nzuri.” amesema na kuongeza

Hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassani Suluhu amelisisitiza sana hili kwamba ni Vizuri na inapendeza watu wakafanya mazoezi. ” Amesema

Amesema kuwa kufanya mazoezi ni vizuri zaidi sio mpaka Daktari akuambie au akuandikie kuwa ufanye mazoezi, lakini wafanyakazi wa Chuo Cha Usafirishaji cha NIT wamelitambua hilo na wameanza kuhamasisha kufanya mazoezi.

Advertisement

Amesema kuwa viongozi wa juu wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji wameona wahamasishe wafanyakazi wenzao kufanya mazoezi kwa kila baada ya robo mwaka ili kujiimarisha kimwili, kiakili na kitamaduni wa kufanya mazoezi kila siku.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kufanya mazoezi kwani ni mazuri kwa kila mtu. “Kwahiyo natoa wito kwa watanzania wote kwamba tufanye mazoezi mazoezi ni dawa ya kuweka mwili wako ukiwa katika afya njema na kwa kufanya mazoezi tunaweza kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza na mangonjwa mengine ambayo hayana msingi wa kukupata.

Kwa upande wa Mkufunzi wa Michezo Chuo Cha NIT Agustino Sakwale amesema kuwa michezo ni burudani michezo ni afya kwani watumishi wote wa NIT wameshiriki bonanza la michezo ili kuendelea kulindaa afya zao.

“Ushiriki wa watumishi wa Chuo cha NITutaimarisha afya zao na pia huongeza ati katika utendaji wa majukumu yao.” Amesema Sakwale.

Licha ya hao Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Sara Mwakyusa amesema kuwa amefurahishwa na bonaza kwani watumishi wanatakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara kwa ajili ya afya zao.

“Mazoezi haya ni mhimu na mazuri kwani yanawajuisha wote pamoja, tunafurahi pamoja, inatuweka pamoja na tunashirikiana pamoja.” Amesema Sara.

Michezo mbalimbali imeshindaniwa katika kuadhimisha bonanza hilo ikiwemo ya Kukimbiza Kuku, kukimbi na yai kwenye kijiko, kukimbia na maguni, mpira wa miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa wavu na mbio za vikwazo na kutunga uzi kwenye sindano huku ukikimbia. Washindi wa michezo hito walijishindia zawadi kemkem zikiwamo pesa taslimu

Advertisement