Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Changamoto wanayopata mashabiki kwa Mkapa

MVUA zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, zinawafanya mashabiki wa Simba na Yanga waliofika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuwa na wakati mgumu wa ‘kujistili’ wasiloane.

Mvua ikiacha kunyesha mashabiki wanakuwa wengi pembeni mwa ukuta wa uwanja huo, ikianza kunyesha wanarejea tena.

Kuna baadhi ya mashabiki ambao walikuwa kwenye foleni ya kuingia uwanjani katika geti D baada ya kuanza kunyesha mvua wakakimbia.

Kwa mashabiki ambao wanaendelea kukomaa kwenye mvua wanaonekana kuwa na imani kubwa ya mchezo huo kuchezeka jioni, ingawa wapo wanaoamini inaweza ikawa ngumu kama mambo yakiendelea hivyo.

Lakini kwa wale ambao wamefanikiwa kuingia uwanjani vinasikika vikipigwa vigoma na mavuvuzela kama kawaida.

Geti D la kuingilia Uwanja wa Benjamin Mkapa, idadi ya mashabiki imeanza kuongezeka kwa kasi, tofauti na mwanzo na tayari baadhi yao wameingia ndani.

Mashabiki hao wamefika kwenye uwanja huo kwa ajili ya kuzisapoti timu zao kwenye dabi ya Kariakoo ambapo Simba ndio mwenyeji wa mchezo huo, unaotarajiwa kuanza saa 11:00 jioni.

Kutokana na hali ya hewa kuwa ya mvua, hakuna nyomi ya mashabiki kama inavyozoeleka kwenye mechi hizo, kwani hata wanaoingia hakuna presha ya kusukumana.

Pamoja na hilo mashabiki hao hawaonyeshi kutambiana ingawa wale ambao Wana mzuka sana baadhi ambao wameonekana vifua wazi, huku shabiki wa Simba mmoja akiwa amebeba jeba jekundu lilioandikwa Chama, Onana,Phiri Asante Mo. Simba unyama mwingi.