Cannavaro pekee aliyekuwa uwanjani Yanga ikipigwa mkono na Simba 2012

Muktasari:
Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi mabao mawili, Felix Sunzu, Juma Kaseja na marehemu Patrick Mafisango kila moja alifunga bao moja.
Dar es Salaam. Kuelekea katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakao chezwa Agosti 23, Uwanja wa Taifa ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’ pekee aliyesalia katika kikosi cha Yanga kilichofungwa na Simba mabao 5-0, Mei 6, 2012.
Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi mabao mawili, Felix Sunzu, Juma Kaseja na marehemu Patrick Mafisango kila moja alifunga bao moja.
Safu ya ulinzi wa Yanga iliongozwa na kipa Mghana Yaw Berko, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Seif ‘Kijiko’, Nurdin Bakari, Haruna Niyonzima, Davies Mwape, Rashid Gumbo na Hamisi Kiiza.
Ni miaka mitano sasa imepita tangu kipigo hicho kilichoanza simanzi nzito Jangwani, lakini bado Haroub ‘Cannavaro’ ni nahodha Yanga na Jumatano ataiongoza timu yake kuivaa Simba.
Pia, Haruna Niyonzima alicheza mechi hiyo akiwa Yanga, lakini Jumatano ijayo atakuwa akichezea Simba.
Upande wa Simba wenyewe itaingia katika mchezo huo ikiwa na wachezaji watatu waliocheza mechi ya Mei 6, lakini wachezaji hao wote waliondoka na kurejea tena.
Wachezaji hao ni Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto na Emmanuel Okwi.
Vikosi vilivyoanza:
Simba: Juma Kaseja, Nassor Masoud, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kelvin Yondan, Patrick Mafisango, Uhuru Suleiman, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Emmanuel Okwi.
Kocha: Milovan Cirkovic
Yanga: Yaw Berko, Nsajigwa Shadrack, Oscar Joshua, Athumani Iddi, Nadir Haroub, Juma Seif, Nurdin Bakari, Haruna Niyonzima, Davies Mwape, Rashid Gumbo na Hamisi Kiiza.
Kocha: Konstadin Papic