Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bondia Mwakinyo kuzichapa na Mjerumani kuwania ubingwa WBO

Muktasari:

Pambano hilo la uzito wa Super Welter, limepangwa kufanyika Machi 21 kwenye ukumbi wa Bayehalle, Wuppertal, Nordrhein, Westfalen nchini Ujerumani chini ya promota Ingo Volckmann wa kampuni ya Agon Sports.

Dar es Salaam. Hatimaye bondia Hassan Mwakinyo amefanikiwa kupata pambano kuwania ubingwa wa WBO dhidi ya bondia Jack Culcay wa Ujerumani.

Pambano hilo la uzito wa Super Welter, limepangwa kufanyika Machi 21 kwenye ukumbi wa Bayehalle, Wuppertal, Nordrhein, Westfalen nchini Ujerumani chini ya promota Ingo Volckmann wa kampuni ya Agon Sports.

Promota huyo tayari amewasiliana na Jay Msangi ambaye mara ya mwisho aliandaa pambano la lisilo la ubingwa dhid ia bondia kutoka Ufilipino, Arnel Tinampay na kushinda kwa pointi.

Pambano hili litasimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa la Ujerumani ambapo aliyetafuta pambano hilo (match maker) ni Hagen Doering na tiketi zinapatikana kupitia mtandao www.ticketmaster.de.

Mbali ya Mwakinyo kuzichapa siku hiyo, waandaaji wameandaa mapambano mengine sita ambapo bondia       Bjoern Schicke atazichapa na Diego Natchoo kuwania ubingwa wa uzito wa middle wa EBU European Union Middle, pambano ambalo linasimamiwa na Peter Stuck wakati bondia Vincenzo Gualtieri atapambana na Alexander Pavlov katika pambano la ubingwa wa Ujerumani wa zito wa middle wakati  bondia Artur Mann atazichapa na Tamas Lodi kuwania ubingwa wa uzito wa cruiser.

Mapambano mengine yatawahusisha mabondia Adam Amkhadov atakaye pambana na Marco Miano katika uzito wa middle huku Jama Saidi atapambana na Viktar Murashkin katika uzito wa middle na bondia Fabian Thiemke atapigana na Vasyl Kondor katika uzito wa light heavy.

Taarifa zimesema kuwa Mwakinyo atatakiwa kupambana tena na Culcay endapo atashinda pambano hilo Tanzania na kama atachapwa, basi pambano la marudiano litafanyika nchini jerumani.

Msangi alithibitisha kupoke taarifa hiyo na kusema ni fursa kwa Mwakinyo kuwania ubingwa wa chama cha WBO.

Alisema kuwa nafasi aliyopata Mwakinyo ni kubwa sana na endapo atashinda, basi atawania ubingwa wa dunia.

Mwakinyo hakuweza kupatikana kuzungumzia pambano hilo kutokana na simu yake kutopatikana.