Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BM aanza, Mayele asubiri Yanga ikiivaa Geita

Mwanza. KOCHA wa Yanga, Nasredinne Nabi amepangua kikosi chake kitakachoanza leo dhidi ya Geita Gold huku mawinga Bernad Morrison, Denis Nkane na mshambuliaji Haritier Makambo wakipewa kazi maalum ya kuimaliza Geita.

Yanga itaikabili Geita Gold kuanzia saa 10 jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza huku ikisaka pointi tatu za kuendelea kuwaweka kileleni mwa Ligi Kuu na kuendelea kuboresha rekodi yao ya kucheza bila kufungwa.

Katika mchezo wa leo Kocha Nabi amepangua kikosi chake kwa kupumzisha wachezaji sita walioanza kwenye mchezo uliopita dhidi ya KMC bao waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Feisal Salum dakika ya 80 akitokea benchi.

Mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Mayele ambaye alikosekana mchezo uliopita leo amerejea lakini ataanzia benchi pamoja na mastaa wenzake waliozoeleka kuanza kikosi cha kwanza, Yanick Bangla, Djuma Shaban, Aziz Ki, Tuisila Kisinda, Jesus Moloko na Joyce Lomalisa.

Nyota walioanza dhidi ya KMC na wamepanguliwa leo ni nahodha Bakati Mwamnyeto ambaye ana matatizo ya kifamilia, Dickson Ambundo (siyo sehemu ya mchezo wa leo), Yanick Bangala, Gael Bigirimana, Tuisila Kisinda na Aziz Ki ambao wanaanzia benchi.

Nafasi za mastaa hao zimechukuliwa na  Kibwana Shomari, Zawadi Mauya, Feisal Salum, Denis Nkane na Bernad Morrison ambao hawakuanza katika mchezo uliopita.

Kikosi cha Yanga leo ni Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Farid Mussa, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Zawadi Mauya, Feisal Salum, Salum Abubakar 'Sureboy', Haritier Makambo, Denis Nkane na Bernad Morrison.

Kikosi cha akiba: Erick Johora, Djuma Shaban, Yanick Bangala, Joyce Lomalisa, Gael Bigirimana, Jesus Moloko, Aziz Ki, Fiston Mayele na Tuisila Kisinda.