Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Berkane yatuma wanne Dar

Muktasari:

  • Simba itaanzia ugenini kuvaana na Berkane Mei 17 kabla ya kurudiana nao Kwa Mkapa Mei 25 kombe likiwa uwanjani, huku taarifa zikisema tayari Wamorocco wametuma mashushushu wanne ili kuipeleleza vya kutosha Simba katika mechi za ligi kabla ya kuwasubiri kwa fainali ya kwanza ugenini.

MAMBO yameanza kuchangamka baada ya RS Berkane ya Morocco itakayocheza na Simba katika mechi mbili za fainali za Kombe la Shirikisho Afrika kudaiwa kutuma watu wanne ili kuja nchini kuisoma ikila viporo vya Ligi Kuu Bara, ambapo leo jioni itaumana na Pamba Jiji, Uwanja wa KMC.

Simba itaanzia ugenini kuvaana na Berkane Mei 17 kabla ya kurudiana nao Kwa Mkapa Mei 25 kombe likiwa uwanjani, huku taarifa zikisema tayari Wamorocco wametuma mashushushu wanne ili kuipeleleza vya kutosha Simba katika mechi za ligi kabla ya kuwasubiri kwa fainali ya kwanza ugenini.

Simba imetinga fainali kwa kuing’oa Stellenbosch ya Afrika Kusini kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0 wakati wapinzani wake waliitoa CS Constantine ya Algeria kwa jumla ya mabao 4-1, na katika kuhakikisha wanaisoma kwa undani Berkane imetuma mashushushu hao wanne akiwemo mtathmini wa mechi kupitia video (video analyst).

Hii inaweza isiwe taarifa nzuri kwa Simba, kuwa ikae chonjo leo itakapovaana na Pamba Jiji katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwani ufundi wowote itakaoufanya pale KMC itawapa akili mashushushu hao ambao hata hivyo hawakutajwa majina.

Mbali na ‘video analyst’, wengine waliokuja kuisoma Simba ni pamoja na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo iliyopo Ligi Kuu Morocco (Batola Pro) na kigogo mmoja wa Wizara ya Michezo nchini humo.

“Wawili wataondoka baada ya siku chache, lakini wengine wawili wataondoka Mei 12 baada ya mechi dhidi ya KMC,” chanzo chetu makini kimelidokeza Mwanaspoti na kuongeza:

“Wanataka kuisoma Simba hadi katika mechi dhidi ya KMC kabla ya kwenda kukutana na Waarabu Mei 17, lakini watatumia nafasi hiyo kuweka mambo sawa kabla ya kikosi hicho kuja nchini kwa fainali ya Mei 25.”

Simba inashuka uwanjani kuvaana na Pamba Jiji ikiwa ni baada ya kutoka kushinda dhidi ya Mashujaa na JKT Tanzania, ikiwa ni viporo wakati ikiwajibuka katika michuano ya CAF.