Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Benchi linampa presha Asukile

Muktasari:

  • Alisema sio kitu kigeni kwa Tanzania Prisons kupitia nyakati za kupambania kuepuka kushuka daraja kwani iliwahi kutokea  msimu wa 2022/23 akiwa nahodha ambako ilinusurika kupitia mechi za mtoano. Pia msimu wa 2014/15 kipindi yupo Kagera Sugar iliwahi kumkuta.

NAHODHA wa zamani wa Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amesema hajawahi kupata presha kubwa kama anayokutana nayo sasa akiwa benchini katika majukumu ya umeneja, tofauti na kipindi alichokuwa anacheza uwanjani.

Alisema sio kitu kigeni kwa Tanzania Prisons kupitia nyakati za kupambania kuepuka kushuka daraja kwani iliwahi kutokea  msimu wa 2022/23 akiwa nahodha ambako ilinusurika kupitia mechi za mtoano. Pia msimu wa 2014/15 kipindi yupo Kagera Sugar iliwahi kumkuta.

“Kitu kinachonipa presha nikiwa benchi ni kutazama matukio moja kwa moja, wakati mwingine akili inanijia ningekuwa uwanjani ningefanya hiki na kile, ingawa nafahamu kabisa kwamba wachezaji wanajitoa wakati mwingine presha ikizidi kwao wanaweza wakatoka mchezoni,” alisema mkongwe huyo na kuongeza;

“Mechi ambayo tulicheza na JKT Tanzania nilishindwa kumalizia nikatoka benchini na kwenda vyumbani, nikaanza kulia maana nikiwa na hasira lazima nilie sana ndipo nikae sawa, nashukuru Mungu matokeo yalikuwa mazuri kwa upande wetu, tulishinda kwa mabao 3-2.”

Asukile kwa uzoefu alionao, anawashauri wachezaji kwa sasa kutambua timu inawahitaji na hawana namna nyingine zaidi ya kujitoa ili kushinda mechi tatu zilizosalia dhidi ya Coastal Union, Yanga na Singida Black Stars.

Asukile alikuwa kati ya wachezaji waliodumu muda mrefu katika kikosi cha Tanzania Prisons kabla ya kustaafu huku msimu huu akipewa majukumu ya umeneja wa timu hiyo.

Kwa mara ya kwanza alisajiliwa msimu wa 2009-2010 kisha akaondoka kwenda kujiunga na Kagera Sugar aliyoitumikia kuanzia 2010 hadi 2015, akarejea Tanzania Prisons 2016 hadi 2024 alipostaafu kucheza.

Kwa sasa Tanzania Prisons inakamata nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 27 huku ikibakiza michezo mitatu, inapambana isishuke daraja kwani nafasi iliyopo si salama.