Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki wa Serengeti Boys hatihati kuivaa Uganda

Muktasari:

Kipigo cha mabao 5-4 kutoka kwa Nigeria kimeiweka Serengeti Boys kwenye nafasi ngumu ya kufuzu nusu fainali ambapo sasa inahitajika kushinda mechi zake mbili zinazofuata dhidi ya Uganda na Angola

Dar es Salaam.Beki wa kati wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 'Serengeti Boys', Ally Rutibinga huenda akaukosa mchezo pili wa mashindano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON U17) kesho dhidi ya Uganda kutokana na majeraha.

Beki huyo alipata majeraha hayo kwenye mchezo uliopita wa ufunguzi dhidi ya Nigeria ambao Serengeti Boys ilipoteza kwa kipigo cha mabao 5-4 matokeo yanayoilazimisha kusaka ushindi kwenye mechi mbili zilizobakia dhidi ya Uganda na Angola ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa vijana wa umri huo.

Kocha wa Serengeti Boys, Oscar Mirambo alisema tangu Rutibinga alipopata majeraha hayo, bado hajawa fiti kwa asilimia mia moja jambo linalomweka kwenye nafasi finyu ya kucheza kesho.

"Mchezaji mmoja aliumia ambaye ni beki wa kati (Ally) na jioni hii amejaribu kufanya mazoezi kidogo jioni hii lakini hali yake bado haijawa nzuri sasa tunasubiri tathmini ya daktari na kuona kama atacheza au vinginevyo

Lakini vijana wote waliobakia wako vizuri na tunaomba Mungu waweze kuamka vizuri tayari kwa mchezo," alisema Milambo akizungumzia maendeleo ya Rutibinga.

Mirambo alisema pamoja na Rutibinga kutokuwa na uhakika wa kucheza, nyota waliobaki wapo tayari kwa ajili ya pambano hilo la kesho na wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Hofu ya kumkosa Rutibinga inakuja katika kipindi ambacho benchi la ufundi la Serengeti Boys linahaha kurekebisha safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa ikiyumba kwenye kila mchezo inayocheza.

Udhaifu wa safu ya ulinzi ya Serengeti Boys ulijidhihirisha kutokana na makosa mengi iliyoyafanya kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Nigeria iliporuhusu mabao matano.

Lakini kabla ya hapo, Serengeti Boys iliruhusu jumla ya mabao 13 katika mechi tano za mashindano ya kirafiki iliyocheza huko Uturuki na Rwanda kabla ya kuanza kwa fainali za Afrika kwa vijana wa umri huo.