Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Mkongo ajishtukia Dodoma Jiji

Beki Pict

Muktasari:

  • Lulihoshi aliyejiunga na timu hiyo msimu huu kupitia dirisha kubwa la usajili kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Tabora United na ameshatumika katika mechi sita za Ligi Kuu Bara akifunga pia bao moja dhidi ya JKT Tanzania kwa mkwaju wa penalti katika mchezo uliopigwa Oktoba 27, mwaka huu.

BEKI wa kati raia wa DR Congo, Heritier Lulihoshi ni kama amejishtukia baada ya kusema anahitaji muda zaidi wa kuonyesha kiwango chake, licha ya kukiri kuna ushindani mkubwa wa namba kutoka kwa wenzake.

Lulihoshi aliyejiunga na timu hiyo msimu huu kupitia dirisha kubwa la usajili kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Tabora United na ameshatumika katika mechi sita za Ligi Kuu Bara akifunga pia bao moja dhidi ya JKT Tanzania kwa mkwaju wa penalti katika mchezo uliopigwa Oktoba 27, mwaka huu.

Akizungumza na Mwanaspoti, beki huyo alisema alichelewa kutumika katika michezo ya mwanzo wa msimu kutokana na vibali vyake vya kazi kuchelewa, lakini kwa sasa anakwenda sambamba na wenzake na bila shaka benchi la ufundi litaendelea kumpa muda.

Alisema hana hofu kwa sababu silaha kubwa ni kujituma na kuonyesha uwezo pale unapoaminiwa, hivyo, anaendelea kujifunza kwa wenzake wanaompa changamoto ya ushindani wa namba kwa masilahi ya klabu hiyo.

“Nafasi ninayocheza ushindani ni mkubwa, lakini nafanya kila kitu kulingana na uwezo wangu na kuwaunga mkono wenzangu tukiwa pamoja ndani ya uwanja hata nisipoanza kikosi cha kwanza, mwisho wa siku maamuzi ni ya kocha na lazima tuyakubali na kuyaheshimu,” alisema Lulihoshi na kuongeza;

“Kipindi ninachopitia kinanipa nguvu kujituma zaidi ili nikipata nafasi niwe tayari na niwe fiti muda wote, kila kitu kinahitaji utulivu wa akili na kujitunza, kwahiyo naendelea kufanya mazoezi binafsi najua ipo siku nitapata muda na kuaminiwa ili kuisaidia timu yangu,”

Beki huyo alitamba kikosi hicho ni kizuri na kinakwenda sawa kutokana na matokeo waliyopata katika mechi 13 ikikusanya pointi 16, huku akilipongeza benchi la ufundi na kuwataka nyota wenzake kujituma pale anapopewa nafasi ili kufikia malengo ya timu mwishoni mwa msimu.