Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Mazembe afichua dili lake Yanga

KEITA Pict

Muktasari:

  • Raha ya mashabiki wa kikosi hicho haiishii kuwaona nyota wao wanaocheza maeneo hayo, lakini kuna mastaa  wengine wanaofanya vizuri na hivyo kuendeleza vaibu Jangwani.

ENEO la ulinzi katika kikosi cha Yanga limekuwa moto kama ilivyo pale mbele ambapo kuna mashinde za mabao zinazowapa raha mashabiki wa timu hiyo yenye makao yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.

Raha ya mashabiki wa kikosi hicho haiishii kuwaona nyota wao wanaocheza maeneo hayo, lakini kuna mastaa  wengine wanaofanya vizuri na hivyo kuendeleza vaibu Jangwani.

Wakati hayo yakiendelea, beki wa TP Mazembe, Ibrahima Keita amekiri kuwa Yanga imemtafuta, lakini bado hawajamalizana ingawa hana shida ya kuitumikia.

Beki huyo ameichezea Mazembe misimu mitatu mfululizo, huku huu akimaliza mkataba wake na klabu hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Keita amesema anaijua Yanga kuwa ni timu kubwa na kwamba hakuna mchezaji anayeweza kukataa kirahisi kuichezea.

Amesema kuwa anamalizia mkataba na Mazembe, lakini anahitaji changamoto mpya na hataki kuongeza mwingine isipokuwa kukipiga sehemu nyingine.

"Ni kweli nimefanya mazungumzo na Yanga, lakini bado hatujafikia makubaliano. Nilikiona kikosi chao katika michuano ya kimataifa ni timu nzuri," amesema.

"Kwa sasa namalizia mkataba wangu, lakini misimu mitatu ni mingi kucheza timu moja. Mipango yangu ni kutafuta changamoto mpya tu."


CHANZO YANGA KUMSAKA

Yanga inasubiri ripoti ya madaktari kujua beki wake,  Yao Kouassi atakuwa nje kwa muda gani, lakini nyuma yake ikaanza hesabu mpya za kumpata Keita.

Endapo Yao atashindwa kuwahi kurudi licha ya kuonekana anajaribu kuchezea mpira mazoezini, lakini Yanga inapiga hesabu kubwa kumsajili beki Ibrahima Keita.

Hesabu za Keita na Yanga hazijaanza sasa, kwani beki huyo jina lake mara ya kwanza liliwasilishwa Jangwani enzi za Kocha Nasredine Nabi ambaye alitaka kumsajili kama angebaki kabla ya kutimka FAR Rabat ya Morocco.

Baada ya Nabi kuondoka Yanga, timu hiyo ilimsajili Yao kuchukua nafasi ya Mkongomani Djuma Shaban, huku Keita akichukuliwa na Mazembe.


KEITA NI NANI

Keita ni raia wa Mauritania mwenye asili ya Mali akiwa na umri wa miaka 23, urefu wa futi 6, anayetumia mguu wa kulia.