Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Basi la Yanga latinga tupu, first eleven yapanda Coaster

Muktasari:

Mabaunsa wa Yanga walionekana kuwa imara kulinda eneo lao ili mashabiki wa Simba wasisogee eneo hilo.

Yanga ndio wamekuwa wa kwanza kufika Uwanja wa Taifa, huku ikisemekana kikosi kinachoanza kitakuja kivingine. Gari lililokuwa limebeba baadhi ya wachezaji wa Yanga lilipitiliza sehemu lililopozoeleka kupaki na kwenda kusimama karibu na mlango wa kuingilia mashabiki wa Simba.

 Saa 7:53 gari aina ya Toyota Coaster liliingia uwanjani huku likiwa limebeba wachezaji ambao wataanza kwenye mechi ya leo.

Wachezaji wa Yanga waliingilia mlango usio rasmi jambo lilozua kelele kwa mashabiki wa Simba.

 Kwenye basi lao kubwa liliwabeba kocha wa makipa Juma Pondamali, meneja wa timu Nadir Haroub 'Cannavaro' baadhi ya wale ambao wanabeba vifaa vya wachezaji.

Baada ya wachezaji wao kushuka na kuingia vyumbani kwenye mlango usio rasmi Cannaro na Pondamali waliwafuata na kuingilia mlango huo.

Mabaunsa wa Yanga walionekana kuwa imara kulinda eneo lao ili mashabiki wa Simba wasisogee eneo hilo.