Barbara: Moyo wangu mzito sana

Saturday September 11 2021
barba pic
By Mwandishi Wetu

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amemlilia Zakaria Hans Poppe aliyefariki Dunia jana usiku katika hospitali ya Aga Khan alipokuwa anapatiwa matibabu.

Kupitia Instagram Barbara ameonyesha masikitiko juu ya Mjumbe huyo wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye walikuwa wakisafiri pamoja katika mechi mbalimbali za timu hiyo kimataifa.

"Leo moyo wangu ni mzito sana Mungu ailaze roho ya marehemu Zakaria Hans Poppe mahali pema peponi. May the Lord Almighty rest your beautiful soul in eternal peace, Mapenzi ya Mungu yatimizwe,"

Advertisement