Barabara Kwa Mkapa itifaki imezingatiwa

MOJA ya vitu ambavyo vimetiliwa umakini wa hali ya juu maeneo ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mechi ya Watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ni barabara.

Utaratibu wa kuingia kwenye uwanja wa Taifa kwa usafiri wa magari ni kupitia njia moja tu ile inayotokea Uhasibu na Chang’ombe.

Barabara inayotokea Chuo Kikuu kishiriki cha DUCE kwa leo haitumiki na imefungwa kwa kuwekwa gari kubwa lilillopaki katikati ya barabara hio hali ambayo hakuna gari wala bajaji inaweza kupita.

Sehemu ya kuingilia uwanjani hapo kwa siku ya leo ambayo ni barabara ya kutokea uhasibu ambapo kumeweka geti maalumu kwaajili ya ukaguzi.

Eneo hilo kuna asikari ambao wanakagua magari na kuruhusu yale yenye ‘sticker’ maalumu za kuingilia uwanjani hapo huku magari mengi yakikwama nje.