Bangala, Shomari warejea Yanga ikiivaa Geita

KOCHA Nasreddine Nabi amewarudisha kikosini wachezaji Shomari Kibwana na Yanick Bangala kwenye mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold.
Bangala na Kibwana hawakupata nafasi ya kucheza kwenye mchezo wa mwisho wa ligi Yanga ikiivaa Azam FC kutokana na sababu mbalimbali.
Wawili hao leo wameanza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga sambamba na wengine tisa.
Langoni atakywepo Djigui Diarra huku mabeki wakicheza, Shaban Djuma, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Kibwana.
Viungo ni Zawadi Mauya, Bangala na Said Ntibazonkiza Farid Mussa na Deus Kaseke watacheza kama mawinga huku Fiston Mayele akipangwa eneo la mshambuliaji wa kati.
Kwenye benchi wapo Abultwalib Mshery, Ibrahim Bacca, Yassin Mustafa, Abdalah Shaib, Dickson Ambundo, Balama Mapinduzi, Chrispin Ngushi, Herietie Makambo na Jesus Moloko.