Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya kuifunga Simba, Chirwa arushia kijembe vigogo

Muktasari:

  • Chirwa amesema mbali na kuifunga Simba alipanga pia kuifunga Yanga ambayo ilinusurika kidogo sambamba na Azam ambazo amejipanga kuzitafuta msimu ujao.

MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Obrey Chirwa ameeleza maana ya ushangiliaji wa bao alilowafunga Simba akisema anawarushia kijembe kuwajibu ambao walimkataa kwa kumuona kuwa ni mshambuliaji mzee.

Kwenye mchezo wa juzi, Kagera ikiwa nyumbani, Chirwa aliisawazishia bao wakati ikiwa nyuma na kuufanya mchezo kumalizika kwa sare ambapo baada ya kufunga alikwenda kushangilia kwenye kibendera akishika mti huo na kutembea mithili ya babu mwenye mkongojo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chirwa raia wa Zambia, amesema ushangiliaji ule ulikuwa ujumbe kwa timu kubwa hapa nchini ambazo ziliwahi kumwacha na kumkataa kwa madai amezeeka.

Chirwa amesema mbali na kuifunga Simba alipanga pia kuifunga Yanga ambayo ilinusurika kidogo sambamba na Azam ambazo amejipanga kuzitafuta msimu ujao.

"Hizo timu ziliniacha baadhi na nyingine zikadai mimi mzee lakini nilisema kila nitakapokutana nao nataka kuwafunga ili wajue mimi sio mzee na nikabahatika kuwafunga Simba," amesema Chirwa ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Azam na Namungo.

"Yanga wana bahati sana mechi ya kwanza nilishawafunga waamuzi wakawabeba, nikawakosa mechi ya pili kidogo na bado Azam hapa Tanzania kuna dharau sana watu wakikuzoea. Mimi bado ni mshambuliaji mwenye nguvu nyingi, lakini wao wanakuona mzee dawa yao ni kuwafunga na kuwajibu kama vile ili waheshimu wachezaji."

Chirwa ambaye aliyefunga mabao matano kwenye ligi, amesema timu kubwa zimekumbatia washambuliaji ambao hawajafikia mabao yake huku wakiwa wamezungukwa na viungo bora.