Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz Ki mchezaji bora Oktoba akiwashinda Phiri, Maxi

KAMATI ya tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemtangaza mchezaji wa timu ya Yanga, Stephane Azizi Ki kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu kwa mwezi Oktoba akiwashinda Maxi Nzengeli wa Yanga na Moses Phiri wa Simba.

Azizi Ki ameifungia timu yake mabao mannekatika dakika 278 za michezo mine aliyoichezea timu yake mwezi huu.

Kamati hiyo pia imemtangaza kocha wa Simba Roberto Olivieira kuwa kocha bora wa mwezi baada ya kushinda michezo yote mitatu aliyocheza mwezi     Oktoba akiifunga Tanzania Prisons 1-3, Singida Big Stars mabao 1-2 na Ihefu 2-1.

Robertinho amewashinda Miguel Gamondi wa Yanga, abdulhamid Moalin wa KMC aliongia nao fainali.

Aidha kamati imemtangaza meneja uwanja wa Higland estate mkoani Mbeya Mulale Omar kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi Oktoba.