Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI: Ishu ya mkataba mpya nawaachia Yanga

Muktasari:

  • Ndani ya wiki za karibuni kulizuka tetesi juu ya mchezaji huyo kuwa hajasaini mkataba na baadhi ya watu walidai amesaini mkataba mpya, hivyo kwa kauli hiyo inaonyesha bado hajapewa kandarasi mpya.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Aziz KI amesema kuhusu suala la kuongeza mkataba mpya ishu hiyo anaichia timu hiyo ambayo ameitumikia kwa msimu wa pili.

Aziz KI hadi sasa analingana mabao na Feisal Salum kwenye vita ya ufungaji katika Ligi Kuu Bara kila mmoja akiweka kambani mabao 18.

Akizungumza baada ya timu hiyo kukabidhiwa Kombe la Ligi Kuu Bara, kiungo huyo amesema ni kweli amepokea ofa kutoka nchi mbalimbali, lakini asilimia kubwa anaipa Yanga kusaini mkataba mpya.

Mchezaji ambaye msimu huu amekuwa moto katika kikosi hicho, mkataba wake wa miaka miwili uko ukingoni na awali ziliibuka taarifa kwamba alikuwa ameshasaini dili jipya, lakini hakukuwa na uthibitisho wowote kutoka pande hizo mbili.

Ndani ya wiki za karibuni kulizuka tetesi juu ya mchezaji huyo kuwa hajasaini na wengine wakisema amesaini mkataba mpya hivyo kauli hiyo inaonyesha bado hajapewa kandarasi mpya.

"Ni kweli nimezungumza na kupokea ofa timu nyingi, lakini kipaumbele nawapa Yanga. Nina furaha sana hapa tusubiri msimu uishe tutazungumza kuhusu mkataba," amesema mchezaji huyo aliyetua Jangwani akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast.