Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI aanzia benchi na Watunisia

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefanya mabadiliko machache katika kikosi chake kinachoingia uwanjani leo kucheza na Club Africain ya Tunisia kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo wa marudiano unapigwa katika Uwanja wa Stade Olympique Hamadi Agrebi huku ukitazamiwa kuleta ushindani mkubwa.

Katika mabadiliko hayo kiungo nyota Stephane Aziz KI ambaye alianza mchezo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ameanzia benchi huku Feisal Salum akirudishwa kucheza namba yake 10.

Kwenye kikosi kinachoanza ni Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Yannick Bangala, Khalid Aucho, Salum Abubakar 'Sure Boy', Jesus Moloko, Fiston Mayele, Feisal Salum 'Fei Toto' na Bernard Morrison.

Wachezaji wa akiba ni Abutwalib Mshery, Ibrahim Abdallah Bacca, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Gael Bigirimana, Tuisila Kisinda, Farid Mussa, Stephane Aziz KI na Heritier Makambo.

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikihitaji ushindi au sare ya mabao ili kutinga hatua ya makundi baada ya Novemba 9, kushindwa kutamba ikiwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kufuatia kulazimishwa suluhu.