Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yaipa ahueni Yanga kwa Simba

Muktasari:

Yanga itashuka katika Uwanja wa Sokoine, Alhamisi, kuvaana na Mbeya City, katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Dar es Salaam. Sare ya mabao 2-2 kati ya Simba dhidi ya Azam FC imeifanya Yanga kupumua katika mbio zake za ubingwa msimu huu.

Simba ilijikuta ikilazimisha sare katika mchezo wao wa kiporo, ambao ushindi wa aina yoyote ungewafanya kuwasogelea vizuri Yanga, ambao wanaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi 44.

Yanga inaongoza kwa pointi 44, lakini Simba ilitakiwa kushinda michezo yake mitatu ya viporo ili kuifikia Yanga na kuishusha kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga, lakini kwa sare hiyo, mabingwa hao watetezi sasa watalazimika kushinda mchezo wao ujao wa kiporo dhidi ya Namungo ili kuwa nyuma ya mabingwa wa kihistoria kwa tofauti ya pointi mbili.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere alianza kuipa Simba bao la kuongoza mapema kipindi cha kwanza na kuifanya miamba hiyo ya Kariakoo kwenda mapumziko ikiwa na uongozi wa 1-0.

Kipindi cha pili kilikuwa bora zaidi kwa Azam FC, ambao walibadilika na kuonyesha soka safi la kushambulia.

Kiungo wa pembeni wa Azam FC, Idd Seleman ‘Nado’ aliisawazishia miamba hiyo ya Mbagala kwa kwa shuti kali la mguu wa kushoto lililomshinda kipa wa Simba, Aishi Manula.

Baada ya bao hilo, Simba iliendelea kusaka ushindi wa kufufua matumaini ya kuishusha Yanga kileleni bila mafanikio.

Nado kwa mara nyingine alihusika katika bao la pili kwa kuxcheza vizuri na Ayoub Lyanga, aliyeitanguliza Azam FC.

Lakini makosa ya umakini kwa safu ya ulinzi ya miambva hiyo ya Chamazi, ilimpa nafasi Luis Miquissone kuisawazishia Simba kwa shuti kali la nje ya 18 na kugawana pointin katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Kocha msaidizi wa Azam FC, Vivien Bahati alisema vijana wake walipoteza umakini katika dakika za mwisho na kuwanyima ushindi katika mchezo huo muhimu kwao.

“Tungeweza kuibuka na ushindi, lakini umakini katika dakika za mwisho ulitunyima nafasi ya kupata ushindi,” alisema Bahati.

Kocha wa Simba, Didier Gomes alisema wachezaji wake walikuwa na siku nzuri iliyokosa bahati, huku akiwapongeza wapinzani kuwa na mchezo mzuri na kufunga mabao yasiyo na utata.