Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC yaishusha Geita Gold

Azam FC yaishusha Geita Gold

Muktasari:

  • Klabu ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye uwanja wa Azam Complex.

Klabu ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye uwanja wa Azam Complex.
Mabao ya Azam yamefungwa na Shaban Chilunda dakika ya 45 kipindi cha kwanza kabla ya Idris Mbombo kuiandikia timu hiyo bao la pili dakika ya 82.

Mchezo huo ulianza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu huku Mbeya Kwanza ikicheza kwa tahadhari zaidi kuanzia kuzuia na kuanzisha mashambulizi licha ya kukosa umakini na kusababisha kufungwa mabao hayo.

Katika mchezo wa leo, Azam ilimkosa mshambuliaji wake, Rodgers Kola mwenye mabao tisa aliyekwenda kwao Zambia kwa ajili ya maziko ya baba yake mzazi, Damiano Kola Senior aliyefariki Jumatatu ya Juni 11.

Matokeo haya yanakuwa na faida zaidi kwa Azam kwani baada ya mchezo huo inasogea hadi nafasi ya tatu na pointi 40 na kumshuka Geita Gold iliyopo ya nne na pointi 39 baada ya timu zote kucheza michezo 27.

Kwa Mbeya Kwanza ina kazi kubwa ya kujinasua na janga la kushuka daraja kwani matokeo haya yanaifanya kuendelea kusalia mkiani mwa msimamo na pointi 24 baada ya kucheza michezo 27 ikisaliwa na mitatu tu.

Katika mechi tatu zilizosalia kwa Azam itacheza na Tanzania Prisons Juni 22, Dodoma Jiji Juni 25 na Biashara United Juni 29.

Michezo iliyobaki Kwa upande wa Mbeya Kwanza ni dhidi ya KMC Juni 21, Ruvu Shooting Juni 25 na Simba Juni 29.