Aucho kuikosa fainali CAFCC nyumbani, ugenini

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Afrika(CAF) zinaeleza kuwa endapo mchezaji akikusanya kadi za njano sita ataikosa michezo miwili.

KIUNGO wa ulinzi wa Yanga, Khalid Aucho atakosekana kwenye michezo miwili ya fainali dhidi ya USM Algers ya Algeria baada ya kupewa kadi za njano sita.

Kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Afrika(CAF) zinaeleza kuwa endapo mchezaji akikusanya kadi za njano sita ataikosa michezo miwili.

Aucho alipewa kadi hizo tano kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kuanzia hatua ya makundi na moja kwenye hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal.

Kadi moja alipewa kwenye mechi ya ugenini dhidi ya Club Africain, moja dhidi ya Monastir, dhidi ya Rivers United na mbili alipewa walipocheza na Marrumo Gallants hatua ya nusu fainali.

Jumapili saa 10 kamili jioni Yanga itashuka dimba la Benjamin Mkapa kucheza fainali ya kwanza dhidi ya USM Algers ya Algeria ambao tayari washawasili nchini.