Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aucho, Diarra wasepa na Simba

Muktasari:

  • Wachezaji hao walikutana na wachezaji wa Simba katika uwanja wa ndege walipokuwa wanaenda nchini Moroccco katika kambi ya kujiandaa na msimu mpya.

MASTAA wa Yanga, Khalid Aucho na Djigui Diarra wamepishana na wachezaji wa Simba ambao walikuwa wanaondoka kwenda nchi Morocco kwa ajili ya kambi msimu mpya.

Aucho na Diarra walikuja nchini kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga na leo waliondoka kwenda kwao wakisubili ratiba ya kwenda kambini na wao nchini Morocco.

Aucho alipofika uwanjani hapo alisema kwa kifupi; ”Nimechelewa ndege ila wenzangu nitakutana nao huko huko kambi itakuwepo mimi naenda nyumbani kwanza,”

Upande wa Djigui ambaye alikuwa na wakala wake walifika uwanjani hapo ila nao walikupambana na changamoto ya kushindwa kupita kwenye geti ikionekana kama vile wamechelewa.

Meneja wa mchezaji huyo alisikika akipiga simu kwa mtu wa Yanga aliyefahamika kwa jina la Amani na kumuambia wameshindwa kupita baada ya kuchelewa ndege.

Mwanaspoti liliwashuhudia wawili hao wakihaha kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere Terminal 3 kutafuta njia ya kuondoka nchini.

Aucho anarejea nyumbani kwao Uganda na Djigui anarejea nyumbani kwao Mali baada ya wote kukamilisha usajili Yanga.