Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arajiga pilato wa Simba, Yanga Kwa Mkapa kesho

New Content Item (1)
New Content Item (1)

WAKATI homa ya pambano la watani wa jadi ikianza kupanda kabla ya timu hizo kuvaana Jumapili ya kesho Novemba 5, Bodi ya Ligi imetaja  waamuzi watakaopewa pambano hilo litakalopigwa Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

Imezoeleka mara nyingi majina ya waamuzi wanaopewa pambano hilo hufichwa na kuja kutajwa siku moja kabla na leo Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi  Karimu Boimanda, amewataja waamuzi wane na Kamishna wa ‘Kariakoo Derby’

Ahmed Arajiga ataamua dabi hiyo kama muamuzi wa kati akiwa na wasaidizi Muhamed Mkono na Kassim Mpanga na wa akiba ni Ramdhani Kayoko huku Kamishana wa mchezo ni Hosea Lugano kutoka Lindi

Simba itaikaribisha Yanga ikiwa ni dabi yao ya pili msimu huu wa ligi baada ya ile ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Agosti jijini Tanga, Simba ikibeba ngao hiyo