Andrew afanya kweli michuano ya baiskeli Arusha

ARUSHA. Mwendesha baiskeli chipukizi kutoka Arusha Andrew Massawe amefanikiwa kuibuka mshindi katika mashindano ya mchezo huo wa "Burka Mountain bike" yaliyomalizika asubuhi hii mkoani Arusha.
Massawe amefanikiwa kuwa mshindi baada ya kumalizika jumla ya kilomita 50 akitumia saa 1:52:01 na kuwaacha Noel Solomon aliyefika nafasi ya Pili kwa saa 1:53:12 huku Kelvin Didas akimaliza nafasi ya tatu kwa saa 1:54: 07.
Mashindano hayo ya Burka Mountain bike yamefanyika leo jumapili katika viwanja vya Burka vilivyoko eneo la Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Akizungumzia ushindi wake Massawe alisema kuwa ni Mara ya kwanza yeye kushinda mashindano hayo aliyoshiriki Mara mbili mfululizo.
"Kila nikija kushiriki nakoa hata nafasi tano za juu, lakini tangu huu mwezi umeanza nilijiwekea malengo ya kutaka kushinda na nimefanikiwa sitaachia nafasi hii" alisema Massawe