Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amza kujitafuta upya Kagera Sugar

Muktasari:

  • Nyota huyo amerejea ndani ya kikosi hicho kwa mara ya pili baada ya awali kujiunga nacho Januari mwaka jana kwa mkopo wa miezi sita akitokea Singida Black Stars zamani Ihefu, kisha kuondoka msimu huu na kutua kwa ‘Wauaji wa Kusini’ Namungo.

BAADA ya Klabu ya Kagera Sugar kumrejesha aliyekuwa mshambuliaji wa kikosi hicho raia wa Cameroon, Moubarack Amza kutoka Namungo, nyota huyo ameweka wazi anaenda kujitafuta upya mzunguko wa pili utakapoanza kufuatia kuanza msimu huu vibaya.

Nyota huyo amerejea ndani ya kikosi hicho kwa mara ya pili baada ya awali kujiunga nacho Januari mwaka jana kwa mkopo wa miezi sita akitokea Singida Black Stars zamani Ihefu, kisha kuondoka msimu huu na kutua kwa ‘Wauaji wa Kusini’ Namungo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Amza alisema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakapoanza itakuwa ni nafasi nyingine kwake ya kujitafuta upya baada ya kuanza vibaya msimu huu na Namungo, huku akiwaahidi mashabiki wa Kagera kutarajia mazuri.

“Nahitaji kufanya vizuri zaidi ya hapa, kiukweli msimu kwangu umekuwa mgumu kutokana na changamoto mbalimbali kuanzia ushindani wa nafasi ya kucheza mara kwa mara, lakini hilo nimelichukulia kawaida na naamini limekuwa fundisho kubwa.”

Kwa upande wa kocha wa Kagera Sugar Mmarekani, Melis Medo alisema usajili wa nyota huyo utaongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji la kikosi hicho kutokana na ubora wake, huku akiamini ataleta matokeo chanya kwa kushirikiana na wenzake.

Amza hadi sasa hajafunga bao lolote la Ligi Kuu Bara ingawa msimu bora kwake nchini ambao hata yeye anakiri ulikuwa wa 2022-2023, wakati akichezea kikosi cha ‘Wagosi wa Kaya’ Coastal Union ambao alimaliza msimu kwa kufunga mabao saba.

Katika kipindi chote cha miezi sita aliyoichezea Kagera Sugar alifunga mabao matatu ya Ligi Kuu Bara huku mara yake ya mwisho kufunga ilikuwa ushindi wa timu hiyo wa mabao 3-0, dhidi ya Tabora United, mechi ikipigwa Aprili 17, mwaka jana.

Nyota huyo anaenda kuboresha eneo la ushambuliaji la timu hiyo ambalo limekuwa butu baada ya kufunga mabao 10 tu katika michezo yake 15, huku akiungana na Edmund John kutoka Singida Black Stars na Omary Buzungu aliyetokea Mtibwa Sugar.