Ajibu aaga rasmi Yanga

Muktasari:
- Ajib ameondoka Yanga akiwa wameacha rekodi ya kuwa mchezaji aliyetoa pasi 17 za mwisho na kuifungia timu hiyo mabao saba katika msimu ulioisha.
ALIYEKUWA mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib amesema misimu miwili aliyocheza katika klabu hiyo ilikuwa bora zaidi kwake.
Ajib alijiunga na Yanga kwa misimu miwili akitokea Simba alikorudi na kusaini mkataba wa miaka miwili alisema misimu hiyo ilikuwa bora ndani na nje ya uwanja.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instargram, Ajibu ameandika kuwa Yanga ilikuwa sehemu ya familia kwake.
"Nitoe shukrani zangu za dhati kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wote, kwa kuniamini na kuniunga mkono katika kila jambo.
"Ni mengi nimejifunza na nina amini yatanisaidia kunijenga zaidi kama mchezaji sina mengi zaidi ya kusema asanteni sana," aliandika Ajib na kuwaambia Wanayanga kuwa watakutana wakati mwingine tena.