Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahmed: Hatuna cha kujivunia, tukutane msimu ujao

Siku moja baada ya tuzo kwa waliofanya vizuri msimu wa 2022/23 kutolewa, Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema washahitimisha rasmi msimu.

Kupitia Instagram Ahmed amewapongeza waliotwaa ubingwa na waliopata tuzo na wasimamizi wa Ligi pamoja na waaandaji wa tuzo.

"Kwetu Simba tuwapongeze nyota wetu waliotwaa tuzo hakika wametuheshimisha. Kiujumla kama timu hatuna cha kujivunia sana maana hatujapata tulichokihitaji msimu huu," ameandika Ahmed na kuongeza

"Hii inatupa nafasi ya kujipanga zaidi kwa msimu ujao. Ubingwa unahitaji wachezaji bora na timu imara. Ni jukumu letu viongozi kutafuta wachezaji sahihi na kutengeneza timu madhubuti, na hilo limeshaanza kufanyika kwa umaridadi wa hali ya juu sana," ameandika Ahmed

Meneja huyo ameeleza kiu na shauku kubwa ya Wanasimba ni kuona mataji yanarejea kwenye timu yao kwani wamechoka kelele za jirani

"Timu kubwa kama Simba haipaswi kukaa muda mrefu bila mataji, miaka miwili inatosha ni muda sasa wa kurudisha ufalme na wetu. Tukutane 2023/2024,"