Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

5G yamliza Sultan, asaka beki fasta

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kabla ya mchezo huo, kocha huyo alishinda michezo mitatu mfululizo akizichapa Bunda Queens mabao 2-0, Mlandizi Queens 5-1 na kuibamiza Ceassia Queens 3-1, ikiwa ni michezo pekee ambayo timu hiyo imeshinda msimu huu kati ya tisa iliyocheza kabla ya juzi kukumbana na kichapo.

BAADA ya kupata aibu ya kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Simba Queens, kocha mpya wa Alliance Girls, Sultan Juma ameitupia lawama safu ya ulinzi ya timu hiyo na fasta kuamua kutafuta beki wa kati kwenye dirisha dogo ili kuokoa jahazi katika mechi zijazo za Ligi Kuu ya Wanawake (WPL).

Kabla ya mchezo huo, kocha huyo alishinda michezo mitatu mfululizo akizichapa Bunda Queens mabao 2-0, Mlandizi Queens 5-1 na kuibamiza Ceassia Queens 3-1, ikiwa ni michezo pekee ambayo timu hiyo imeshinda msimu huu kati ya tisa iliyocheza kabla ya juzi kukumbana na kichapo.

Kocha huyo wa zamani wa Geita Gold Queens, licha ya kukiri ubora na kuzidiwa na Simba, lakini alisema eneo la ulinzi la timu yake bado linafanya makosa hususan kuokoa mipira ya vichwa, huku akiahidi kulifanyia kazi wakati wa mapumziko ya ligi.

“Bado tuna changamoto kwenye eneo la ulinzi tunashindwa kujilinda vizuri unaona leo tumepoteza kwa mabao mengi maana yake beki yetu ilikuwa dhaifu, tumeingia kwenye mtego wao waligundua tuna udhaifu katika ulinzi wa kati,” alisema Juma na kuongeza;

“Tunakwenda kufanyia kazi hilo kutengeneza beki yetu na tutaongeza mtu ili aje kutusaidia katika eneo hilo. Dirisha dogo tunaongeza watu kama mlivyoona ili tuongeze ubora na sisi twende tukashindane na wenzetu.”

Juma aliwaomba mashabiki wa timu hiyo na wa mkoa wa Mwanza kutokatishwa tamaa na matokeo hayo kwani ubora wa Simba unafahamika, huku akiwaomba waendelee kuiunga mkono ili ipambane na kumaliza kwenye nafasi za juu.

“Tumefungwa mabao mengi lakini ndiyo mpira.”