29 wa kigeni wakoleza utamu BDL

Muktasari:
- Idadi ya nyota hao imekuwa ikiongezeka na wamesajiliwa katika timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo na waliopo hadi sasa ni 29.
USHINDANI na uwepo wa nyota wa kigeni katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), umeifanya izidi kuimarika na kuwa moja ya zinazoongoza kwa ubora Ukanda wa Afrika Mashariki.
Idadi ya nyota hao imekuwa ikiongezeka na wamesajiliwa katika timu mbalimbali zinazoshiriki ligi hiyo na waliopo hadi sasa ni 29.
Wachezaji hao wanatoka katika timu za Dar City, Srelio, DB Oratory, Savio, Pazi na upande wanawake ni DB Oratory, DB Lioness na Pazi Queens
Dar City ilisajiri wachezaji wanne ambao ni Victor Mwoka (Kenya), Jamel Marbuary (Marekani) na Clinton Best (Nigeria).
Mchezaji Larry Mve (Gabon), Dan Kola (Congo), Junior Lousisi (Gabon) na Kabangu Mrc (Congo), wamesajiliwa na timu ya Srelio
DB Oratory imewasajiii Thitenkas Chad (Congo), Kakumbuka Henock (Congo), Hassan Kabanda (Uganda) na Oswald Bera (Congo).
Savio imewasajili Ntibonela Bukeng (Congo), Chelord Kabantu (Congo), Ludovick Zentang (Comoro), huku Kurasini Heat ikiwa na Zadock Emmanuel (Kenya) na Tshiband Anachet (Congo).
Kwa upande wa timu ya Pazi ina Robert Tasire (Uganda), Soro Geofrey (Uganda), Yang Ugweno (Kenya) Trevor Petar (Kenya), Sam Agutu (Kenya
Kwa upande wanawake, Pazi Queens imewasajili Marline Salumu (Congo), Veronica Aluvel (Sudan) na Chantal Dunia (Congo).
DB Lioness imemsajili Taudencia Katumbi (Kenya) Lawender Obinda (Kenya), Sokouudjou Michele (Comoro), Christaian Akinyi (Kenya) na Cynthia Wafula (Kenya).
Timu ambazo hazina wachezai wa kigeni upande wanaume ni KIUT, Vijana ‘City Bulls’, Mgulani JKT, ABC na JKT na kwa wanawake ni Ukonga Queens, Twalipo Queens, Vijana Queens.