Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga mpo? Waziri Jr anaanzia kwenu

Dodoma Jiji yamng'oa Tunisia Waziri Jr

MABOSI wa timu ya Dodoma Jiji FC, walilazimika kupanda ‘mwewe’ hadi nchini Tunisia ili kumsainisha mkataba mshambuliaji wao mpya Waziri Junior, aliyekuwa kwenye majaribio nchini humo.

 Mshambuliaji huyo ambaye walikaribia kumnasa dakika za mwisho kwenye dirisha kubwa la usajili lililopita, alikwenda nchini Tunisia kwa majaribio katika moja ya timu inayoshiriki ligi kuu ya Tunisia (Ligue 1), bado hatma yake ya kusajiliwa na timu hiyo haijulikani.

Kutokuwa na uhakika wa kusajiliwa na timu ya nchini humo, ndio kuliwafanya mabosi wa Dodoma Jiji kumpandia ndege hadi Tunisia, kwa lengo la kumuwahi kabla hajarudi nchini wakihofia kuwahiwa na timu nyingine ambazo zilikuwa zinamuwinda kwa karibu.

Mtedaji mkuu wa timu hiyo, Fourtunatus Johnson, ndiye aliyemfuata nyota huyo nchini Tunisia ambapo alimsanisha mkataba na kurejea naye nchini kabla ya kutambulishwa Jumatatu wiki hii, tayari kuanza kazi ya kuifungia mabao timu hiyo.

“Tulijua mapema kwamba Waziri Jr anasakwa na timu nyingi kwenye dirisha hili la usajili, ndio sababu ili kuonyesha uzito zaidi ya wengine, tukaamua kumfuata kabisa nchini Tunisia ambako licha ya kuwa kwenye rada za timu moja ya Tunisia, tulifikia makubaliano ya kuja kwetu, wakati akisubiri hatma ya kule,’’ alisema Johnson.

Moses Mpunga, ofisa habari wa Dodoma Jiji aliliambia Mwanaspoti kuwa, wanatarajia mchezaji huyo, atakipiga kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Yanga na atavalia jezi namba saba, iliyokuwa inavaliwa na David Ulomi waliyemuuza nchini Sudan.

“Baada ya kumnasa Waziri Jr, sasa tunapambania mchakato wake wa kuwa tayari kucheza mchezo wetu na Yanga, ambapo ameanza mazoezi na wenzake ili kuanza kazi, ambapo atachukua nafasi ya David Ulomi tuliyemuuza Al Hilal ya Sudan,’’ alisema Mpunga.