Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

#WC2018: Patrick Viera aitabiria Ufaransa kucheza fainali

Moscow, Russia. Kiungo wa zamani wa Ufaransa na Arsenal ya England, Patrick Vieira ameitabiria Les Blues kutinga fainali ya Kombe la Dunia 2018, itakayopigiwa, Julai 15, mwaka huu katika dimba la Luzhniki lenye uwezo wa kuchukua mashabiki 81,000 Khamovniki jijini Moscow.

Viera ambaye kwa sasa ni Kocha wa klabu ya Nice, alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichobeba ndoo mwaka 1998 na Kombe la Euro 200, kabla ya kuiongoza Arsenal, kutwaa ubingwa wa EPL msimu wa 2003/04 bila kufungwa maarufu kama 'The Invincibles' chini ya uongozi Arsene Wenger.

Kiungo huyo kisiki, anaamini kikosi cha Didier Deschamps, ambaye alikuwa nahodha wa Les Blues katika ule usiku wa Paris, ni wakali kinoma na kwamba baada ya kuitandika Argentina 4-3 katika mchezo wa kwanza wa hatua hii ya mtoano, wamethibitisha kuwa hakuna wa kuwazuia.

"Tunaweza kuzungumzia kampeni yao kwa namna tofauti na sauti tofauti, lakini ni kwamba hakuna wa kuitisha Les Blues. Nadhani kwa mchezo waliouonesha dhidi ya Argentina ule moyo wa kujituma uliooneshwa na Kylian Mbappe, hatma yake ni kubeba ndoo. Tunaenda fainali," alisema Vieira.

Kauli ya Patrick Vieira anayetajwa kama mmoja wa viungo bora wakabaji waliowahi kutokea katika ulimwengu wa soka, inakuja wakati ambapo Les Blues wanajiandaa kuwakabili Uruguay katika hatua ya robo fainali. Uruguay walifuzu kwa kuwanyoosha Ureno 2-1.