Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waendelea kujishindia zawadi Shinda Ki-Brazil

Muktasari:

Washindi hao walikabidhiwa zawadi zao jana Jumatano ambapo Michael Namenga, Issa Ndingo na Christopher Chengulla walipata ving’amuzi vya DSTV na vifurushi vyake wakati aliyekabidhiwa jezi 16 ni Jackson Fredrick wa Mwanza.

WASHINDI wengine wanne wa Bahati Nasibu ya Shinda Ki-Brazil wamepatikana na kujishindia zawadi za ving’amuzi na jezi.

Hii ni droo ya pili ya shindano hilo linaloendeshwa kwa pamoja kati ya Gazeti la Mwanaspoti na DSTV katika shamrashamra za michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko Brazil.

Wiki iliyopita wasomaji wanne wa Gazeti la Mwanaspoti walijishindia zawadi kama hizo baada ya kushiriki shindano hilo.

Washindi hao walikabidhiwa zawadi zao jana Jumatano ambapo Michael Namenga, Issa Ndingo na Christopher Chengulla walipata ving’amuzi vya DSTV na vifurushi vyake wakati aliyekabidhiwa jezi 16 ni Jackson Fredrick wa Mwanza.

Kwa wiki hii, washindi wa ving’amuzi vya DSTV pamoja na kifurushi kizima cha malipo kwa mwezi mmoja (Compact Plus) ni Sharifu Migui (34), John Kilalago (39) na Mahmud Salum huku mshindi wa jozi moja ya jezi 16 ni Bariki Massawe (38).

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Migui ambaye ni mkazi wa Mikumi Morogoro alisema: “Ninafuraha kushinda kwenye shindano hilo. Ni kitu rahisi kupata kama mtu unashiriki kwani unakuwa umejijengea nafasi ya kutosha endapo unashiriki na mimi nimeshiriki mara nyingi .”

Massawe ambaye ni mkazi wa Tabata Kinyerezi alisema: “Nimefurahi kushinda jezi baada ya kushiriki kwenye promosheni bomba ya Mwanaspoti. Jezi hizo nitatoa zawadi kwa timu yangu ya maveterani inayoitwa Kinyerezi Veteran.”

Huku Kombe la Dunia likiendelea, Mwanaspoti kupitia kwa Mwandishi wake Edo Kumwembe aliyepo Brazil itaendelea kuwapa makala na habari mbalimbali za matukio kuhusiana na Kombe la Dunia.

Akizungumza katika sherehe za kukabidhi zawadi na kutaja washindi wengine, Ofisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited ambao ni wachapishaji wa gazeti la Mwanaspoti, Edward Uisso, alisema kuwa bado kuna zawadi nyingi zimebaki kwa wasomaji ambazo ni runinga tatu zenye ukubwa wa inchi 32, ving’amuzi 24 vya DSTV, seti nne za jezi na fedha taslimu zinazotolewa kila siku kupitia shindano hilo.

“Tumefurahi kuwa mnashiriki. Bado kuna fursa za kujishindia zawadi nyingine nyingi kwa kipindi cha wiki nne zilizobaki, Mwanaspoti na DSTV itaendelea kutambua mchango wenu na kuwazawadia vitu mbalimbali,” alisema.

Aliongeza: “Mwanaspoti linafanya hivi kwa kuwa linawathamini wasomaji wake na wapenzi wa michezo kwa ujumla hivyo limeamua kutoa zawadi hizi katika kipindi hiki kizuri cha shamrashamra duniani kote.”

Ili kuendelea kushiriki, wasomaji wa Mwanaspoti watatakiwa kutuma namba zitakazopatikana kwenye ukurasa huu wa tatu wa Gazeti la Mwanaspoti kwenda namba 15551.