‘Wachezaji wa Tanzania hawajajua utamu wa pesa’

Kocha King Kibadeni katika mazoezi ya vioungo
Muktasari:
Kocha huyo alisema: “Wachezaji wengi wamekuwa na mazoea na wamekuwa wakicheza kawaida na wengine wazembe tu na hii inatokana na wengi wao kutojua utamu wa fedha kupitia soka.
KOCHA wa Ashanti United, Abdallah ‘King’ Kibadeni amesema kuwa laiti kama wachezaji wa Ligi Kuu Bara wangekuwa wamepata kujua utamu wa fedha za soka wangejituma sana na kuacha michezo yao ya kizembe.
Kocha huyo alisema: “Wachezaji wengi wamekuwa na mazoea na wamekuwa wakicheza kawaida na wengine wazembe tu na hii inatokana na wengi wao kutojua utamu wa fedha kupitia soka.
“Mimi nilijituma na kutafuta fedha kupitia soka enzi hizo na ndicho kinachoniweka fiti hadi sasa, wakati wetu pesa ilikuwa ndogo lakini wachezaji walikuwa wanacheza soka la kiwango, sasa kuna fedha nyingi, lakini wachezaji hawajitumi na kuitendea haki fedha hiyo.
“Wachezaji Bongo wanahitaji kujitambua na kuhakikisha wanavuna pesa kupitia soka, kwani soka ni kazi ya muda sema ukiwa mjanja unapostaafu ukiwa na kiwango kizuri unaweza kupata pesa kupitia ukocha kama ninavyofanya mimi,” alisema Kibadeni na kuwataka wachezaji kuamka na kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Kocha huyo pia amewataka wachezaji wasirubuniwe na kuuza mechi bali wafanye kazi.