Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars mbinu kama zote -VIDEO

Muktasari:

  • Amunike aliwataka wachezaji wake kupanda kwa pamoja lakini pia kushuka kwa pamoja huku kila mmoja akiwa anacheza kwa nafasi yake.

KIKOSI cha timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kimeendelea na mazoezi yake ikiwa ni maandalizi ya Fainali za Afcon zitakazoanza kutimua vumbi Misri Juni 21.
Katika mazoezi hayo kocha Emmanuel Amunike alikuwa akitengeneza namna ambavyo timu inaweza kupambana muda wote ndani ya uwanja.
Amunike aliwataka wachezaji wake kupanda kwa pamoja lakini pia kushuka kwa pamoja huku kila mmoja akiwa anacheza kwa nafasi yake.
Zoezi hilo lilionekana kueleweka kwa wachezaji kwani walikuwa wakifanya kile ambacho wanaelekezwa na Amunike.
Baada ya zoezi hilo Amunike aligawa wachezaji timu mbili na kucheza kwa kufuata maelekezo yake.
Stars wanaondoka leo Ijumaa mchana kuelekea Misri ambako kabla ya fainali hizo watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Misri itakayochezwa Juni 13 na Zimbabwe itakuwa Juni 16 mwaka huu.