Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Onyango alizua Simba, agomea safari ya Sudan

Onyango alizua Simba, agomea safari ya Sudan

Muktasari:

  • Beki wa kati wa Simba, Joash Onyango amegomea kwenda nchini Sudan kwa ajili ya kucheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na Al Hilal ya Sudan.

Dar es Salaam. Beki wa kati wa Simba, Joash Onyango amegomea kwenda nchini Sudan kwa ajili ya kucheza mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na Al Hilal ya Sudan.

Kikosi cha Simba kiliwasili salama Sudan jana mchana na Onyango hakuwa katika orodha ya wachezaji 18 waliowasili nchini humo kutokana na sababu ambazo alieleza kabla ya kikosi hicho kuondoka.

Inaelezwa kuwa raia huyo wa Kenya alikuwa katika orodha ya nyota waliotakiwa kusafiri ikiwemo kupata visa na tiketi ya ndege, lakini baada ya mazoezi ya mwisho kumalizika aligomea kwenda nchini humo.

Baada ya mazoezi kuisha, Onyango inaelezwa alimfuata kocha Zoran Minojlovic pamoja na meneja, Patrick Rweyemamu aliyowaomba kufanya nao mazungumzo ya muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda kambini.

Onyango inaelezwa aliwambia Zoran na Rweyemamu kuwa hapendezewi na suala la kuwekwa benchi kama ilivyokuwa katika mechi tatu za kimashindano zilizopita pamoja na baadhi ya stahiki zake za msingi kutokupatiwa hadi leo na uongozi kama walivyokubaliana katika mkataba mpya.

Kabla ya mazungumzo hayo kuisha, Zoran inaelezwa alimuelewa Onyango ila alimwambia anatakiwa kwenda lakini mwenyewe aligoma na kudai anabaki Dar es Salaam hadi masuala hayo mawili yatakapopata ufumbuzi.

Onyango yupo Dar huku akisubiri Simba kutoa uamuzi wa kumtimizia maslahi yake, kupewa nafasi ya kucheza mara kwa mara na kama itashindikana anaweza kuomba barua ya kusitisha mkataba wake.

Tangu kusajiliwa kwa Mohamed Outtara kutoka Al Hilal, amekuwa akicheza kikosi cha kwanza na Henock Inonga katika eneo la beki wa kati, huku Onyango akiishia katika benchi.