Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okrah: Gari limewaka

Okrah: Gari limewaka

NYOTA wa Simba, Augustine Okrah anaamini sasa ni kama gari limewaka kwani ushindi walioupata dhidi ya Geita utasaidia kulainisha mechi ya Kagera leo saa 12 jioni.

Anaamini kwamba kujikwaa kwenye mechi ya Yanga kuliwakwamisha kisaikolojia lakini ushindi wa Geita umewatoa walipokuwa wamegota na sasa ni mbele kwa mbele.

Alisema ushindi umeleta hali ya kujiamini tofauti na ilivyokuwa kabla ya mchezo huo kikubwa ambacho anaamini utakuwa muendelezo mzuri. “Nadhani kila mchezaji aliyepata nafasi ya kucheza ameonyesha ubora wake hadi kufikia mafanikio ya kupata pointi tatu kuhusu suala la kuanza kikosi cha kwanza hilo lipo chini ya benchi la ufundi,” alisema Okrah na kuongeza;

“Kilichokuwa mbele yangu muda wowote ambao nitapewa nafasi ya kucheza nitajitahidi kufanya vizuri zaidi ya mechi iliyopita ili kuisaidia timu kufikia mafanikio ya kupata ushindi.

“Ushindani wa kuwania nafasi ya kucheza katika kikosi cha Simba ni mkubwa.” Staa huyo alisema ndani ya kikosi cha Simba kuna morali na ushirikiano mkubwa.