Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi: Mkija ovyo mtakula nyingi tu

Nabi ashtukia mastaa Yanga

YANGA imefunga mwaka kibabe ikiipiga Dodoma Jiji kwa mabao 4-0, huku kocha wa vinara hao wa Ligi Kuu Bara, Nesreddine Nabi akatoa kauli ya vitisho akisema timu wanazokutana nazo lazima zije na heshima, la sivyo zitakula nyingi sana tu ndani ya 2022.

Akizungumza na Mwanaspoti, Nabi alisema hajashtushwa na ushindi wa kishindo wa timu yake ukiwa ni wa kwanza mkubwa msimu huu kwa vile anajua ubora walionao na kusema moto wao bado kabisa kwenye kufunga mabao.

Nabi alisema ushindi wa juzi walioupata kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ulitokana na makosa ya Dodoma kutocheza na tahadhari juu na makosa waliyofanya yalitengeneza njia ya Yanga kutupia mara nyingi.

“Sina wasiwasi na kikosi changu ingawa hakijafikia ule ubora ninaoutaka mpaka sasa. Ni kama tuna ubora wa asilimia 60 tu, ila wapinzani wetu kuna makosa makubwa waliyafanya,” alisema Nabi.

“Unapocheza na timu kama yetu ukafanya makosa kama yale tutakufunga nyingi tu, uwezo huo tunao. Ila tulijua ni suala la muda tu kushinda kwa mabao mengi kama hivi.”

Nabi alisema katika kufunga mwaka anaona kikosi chake kinazidi kuimarika na sasa wanaenda kujipanga kwa hatua ngumu zaidi katika kumalizia duru la kwanza, kisha kuanza lalasalama.

Alisema duru la pili litakuwa mgumu zaidi kutokana na nafasi wanayoishikilia kwenye msimamo wa ligi.

“Hadi sasa tuna timu iliyothibitisha ina ubora wa kuchukua mataji. Kitu ninachofahamu duru la kwanza limebakiza mechi chache ambazo nazo ni ngumu mno,” alisema.

“Tunatakiwa kujiandaa zaidi na ugumu huo, pia kuna mzunguko wa pili ninaouona utakuwa mgumu zaidi, kwani hakuna timu inayotaka kutuachia tushinde kirahisi. Pia hata wao wanataka kutupunguza kasi yetu. Tunaenda kumalizia usajili na kujipanga zaidi kwa ubora. Huu ni msimu tunaohitaji mafanikio makubwa na hatutaki kuwaangusha mashabiki wetu.”

Yanga inasaka ubingwa wa ligi baada ya kuusotea kwa misimu minne baada ya kunyang’-anywa na Simba iliyoipora tangu 2018 baada ya vijana hao wa Jangwani kubeba mara tatu mfululizo 2015-2017, kwa sasa inaongoza ikiwa na alama 29 katika mechi 11.


MSIKIE MAYELE

Kinara wa mabao wa Yanga, Fiston Mayele amesema amepania msimu wake wa kwanza Ligi Kuu kufunga mabao zaidi ili kuiwezesha kubeba ubingwa naye kuwa Mfungaji Bora.

Mayele mwenye mabao matano akilingana na Vitalis Mayanga wa (Polisi Tanzania), George Mpole (Geita Gold), Reliants Lusajo (Namungo) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons), alisema anatamani kutwaa kiatu cha ufungaji hivyo moto wa mabao kwake utaendelea.

“Kila mchezaji hasa anayecheza eneo la ushambuliaji anatamani kila mchezo afunge. Kuna wakati inatokea unashindwa ila kwa msimu huu nitaendelea kufunga sana kila nipatapo nafasi ili kuisaidia timu yangu, nami niweke heshima ya kuwa Mfungaji Bora,” alisema.

Nyota wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa alisema mchezaji huyo anajua kujiweka katika nafasi nzuri ya kufunga, lakini pia kufunga na jinsi ya kuwatoka mabeki, hivyo anawatahadharisha mabeki kujipanga na kuwa naye makini.

“Mayele ni moja ya usajili bora ambao Yanga imeufanya msimu huu, anawasaidia sana. Kuanzia uwezo wake binafsi na hata kitimu anapambana,” alisema Pawasa.