Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msaada wa kodi, hoteli kuwa karantini Diamond Platnumz ni noma

DIAMOND Platnumz sio tajiri namba moja Tanzania. Hakika hawezi hata kuingia kwenye Top 20 ya matajiri wa Tanzania. Lakini kutoa ni moyo sio utajiri. Bosi huyo wa lebo ya Wasafi Classic Baby amefanya jambo kubwa wiki hii.

Amejitolea kusaidia familia 500 kulipia kodi zao za pango kwa miezi mitatu katika kuwapunguzia Watanzania wenzake makali ya maisha katika kipindi hiki kigumu cha janga la corona.

Mondi pia ametoa hoteli yake mpya ya kisasa itumike kama karantini ya watu wanaohisi kuambukizwa corona.

Hii si mara ya kwanza kwa Mondi kurudisha kwa jamii.

Ameshatoa mitaji ya biashara kwa kinamama, bodaboda kwa vijana, kulipia bima za afya, kuchangia matibabu ya wagonjwa wa moyo kwenye taasisi ya Jakaya Kikwete ya Muhimbili, kugharamia safari ya nchini India na matibabu ya msanii mwenzake, Hawa, aliyeimba naye wimbo wa ‘Nitarejea’.

Haya ni machache kati ya mengi, mengi ya kurudisha kwa jamii ambayo Diamond amekuwa mstari wa mbele katika kuyafanya.

Katika umri wake mdogo wa miaka 30, Diamond ameshaishi takribani aina zote za maisha.

Ameishi maisha ya dhiki akilelewa na mama tu bila baba, baada ya wazazi kutengana, katika eneo la watu wa maisha ya chini Tandale, ameishi maisha ya kitajiri, kisupastaa na amefanya mengi kwa jamii yake.

Kuitoa hoteli yake mpya hivi kwa wakati huu itumike kama karantini, mwingine anaweza kuona kwamba “kwanza hamna biashara kipindi hiki cha corona, hata asingeitoa wateja angepata wapi?” Ni kweli hamna biashara ya hoteli kipindi hiki. Hali ni mbaya kutokana na janga la corona. Watu hawasafiri na hata wanaozitumia hoteli kwa mambo yao mengine, saa hii hofu imewajaa kuhusu corona, wanazikacha.

Lakini kama sababu ni hiyo ya kutokuwepo kwa wateja, mbona wamiliki wengine tena wenye hoteli kali zaidi yake Mondi hawajazitoa zao zitumike kuwa karantini? Kwani Mondi pekee anayemiliki hoteli hapa nchini?

Ukipata majibu ya maswali hayo, unaweza kuona ni namna gani Diamond amekuwa mtu wa kujitolea sana. Kutoa ni moyo si utajiri. Katika kipindi hiki kigumu cha janga la corona, maisha ya wengi yanakuwa magumu na sapoti ikipatikana kutoka kwa wenye afadhali ya maisha ni jambo zuri sana.

Tanzania wapo watu wengi wenye utajiri mkubwa zaidi ya Diamond, huu ni wakati wa kuwashika mkono wenzao.

Diamond daima amekuwa mfano katika kuisaidia jamii yake ambayo kwayo amekuwa akiuza kazi zake za sanaa.

Kujitolea kwake kwa jamii kumechangia upendo usio kifani ambao amekuwa akipokea kutoka kwa jamii.

Mifano inaonekana katika matukio yake ya kisanaa au hata apoonekana mahali.

Mamia ya mashabiki wamekuwa wakifurika kuhudhuria na kusapoti kazi zake.

Na kwa wakati huu ambao dunia imepewa mtihani mzito wa janga la corona, kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kumuangukia Mwenyezi Mungu, kumwomba msamaha kwa makosa yetu kwa sababu sisi wanadamu ni wakosaji na kumwomba kwa rehema zake atuondolee mtihani huu. Amina.