Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele arudi Congo

Mayele arudi Congo

STRAIKA nyota wa Yanga, Fiston Mayele anatarajia kuukosa mchezo wa kwanza wa Mapinduzi dhidi ya Taifa Jang’ombe kutokana na kuondoka kikosini humo na anatarajia kuungana tena na timu Januari 7 mwaka huu.

Baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji juzi Ijumaa, Mayele alipanga kuondoka kwenda Congo kuhani msiba wa shemeji yake na ameliambia Mwanaspoti ataungana na timu visiwani Zanzibar baadaye.

Yanga inatarajia kutupa karata yake ya kwanza kwenye mashindano hayo dhidi ya Taifa Jong’ombe Januari 5 katika mechi itakayopigwa Saa2:15 usiku ndani ya Uwanja wa Amaan, mjini Unguja.

Mayele alisema kukosekana kwake kwenye mchezo huo haiondoi Yanga kuibuka na ushindi kutokana na timu hiyo kusheheni wachezaji wenye uchu wa matokeo mazuri kwenye kila mchezo. Yanga ndio watetezi wa michuano hiyo ikipangwa Kundi B ikiwa pia na KMKM.

“Sichezi peke yangu kwenye timu tunacheza wengi na timu imesajili kikosi kipana ikizingatia wingi wa mashindano hivyo natarajia kusikia matokeo mazuri ya kunifariji nikiwa Congo,” alisema Mayele na kuongeza;

“Yanga mipango yetu ni kutwaa kila taji lililo mbele yetu hivyo tunatarajia mambo makubwa kwenye kila mashindano ikiwa ni sambamba na ushindani hilo halitatukatisha tamaa tutapambana mwanzo hadi mwisho lengo ni kuona mashabiki zetu hawakauki furaha hii ni kutokana na namna wanavyotuamini.”