Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kapombe akumbukwa Stars

Muktasari:

Amunike alisema kikosi chake kinahusisha wachezaji watakaoshiriki Afcon na michuano ya awali ya CHAN ndio maana ameamua kutoa nafasi kwa wachezaji waliofanya vizuri.

  NI kweli Kelvin John ‘Mbappe; straika chipukizi wa Serengeti Boys alikwama kuibeba timu hiyo ya taifa ya vijana kwenye Fainali za Afcon U17, lakini kiwango alichokionyesha kimembeba Taifa Stars.

Kocha wa Stars, Emmanuel Amunike jana alitangaza kikosi chake cha awali cha kushiriki Fainali za Afcon 2019 na kuwajumuisha nyota wapya sana kikosini huku baadhi wakiwa chipukizi.

Amunike alisema kikosi chake kinahusisha wachezaji watakaoshiriki Afcon na michuano ya awali ya CHAN ndio maana ameamua kutoa nafasi kwa wachezaji waliofanya vizuri.

Mbali na Mbappe, Mnigeria huyo amewaita pia Claryo Boniface, Fred Tangalu, Ayoub Lyanga, Kassim Hamis, Miraj Athuman na straika anayekipiga Uingereza Adi Yusuph.

Adi Yusuph anayekipiga Solihull Moors iliyomaliza nafasi ya pili katika Ligi Daraja la Pili nchini England ikiwamia kupanda daraja katika hatua ya playoff.

Amunike alisema anajua wengi watashangazwa na kuita wachezaji 39, lakini alisisitiza ameangalia namna walivyofanya vizuri katika klabu zao, pia ikiwa ni maandalizi ya fainali za Afcon na CHAN zinazofanyika mwaka huu.

“Tukitoka Afcon hatutakuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kupiga hesabu za haraka kuelekea katika Chan, ndio maana nimeita idadi hiyo, lakini itasaidia wengine kupata uzoefu na kuibeba timu.”

Akizungumzia maandalizi kuelekea fainali za Afcon zinazotarajia kuanza Juni mwaka huu, alisema anatambua changamoto zake hivyo anataka kwenda kama mshindani na sio mshiriki.

Stars inatarajia kuanza mazoezi Juni Mosi kabla ya kwenda Misri kucheza mechi za kirafiki na Misri na Nigeria ili kujiweka kabla ya mashindano ya Afcon kuanza kutimua vumbi Juni mwaka huu. Kikosi cha wachezaji 32 ndicho kitaondoka kwenda nchini Misri, huku wachezaji 30 wakiwa ni wazoefu wawili wakiwa ni chipukizi (Kelvin John na Claryo Boniface)

Wachezaji walioitwa Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata (Mbao), Claryo Boniface (Ngorongoro Heroes), Suleman Salula (Malindi), Aron Kalambo (Prisons), Hassan Kessy (Nkana Fc) na Vicent Philipo (Mbao).

Wengine ni Shomari Kapombe (Simba) ambaye alikuwa nje kwa muda mrefu akiuguza jeraha la mguu, Gadiel Michael (Yanga), Abdi Banda (Baroka), Ally Mtoni (Lipuli), Mohammed Hussein (Simba), Agrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Erasto Nyoni (Simba).

Pia kuna David Mwantika (Azam), Ally Ally (Kmc), Kennedy Wilson (Singida) Feisal Salum (Yanga), Himid Mao (Petrojet), Mudathir Yahya (Azam), Yahya Zaydi (Ismailia), Jonas Mkude (Simba), Ibrahim Ajib (Yanga) na Fred Tangaru (Lipuli Fc).

Amunike pia kawaita Frank Domayo (Azam fc), Shaaban Chilunda (Tenerife), Shiza Ramadhan (Enppi), Simon Msuva (Al Jadida), Rashid Mandawa (BDF Xi), Mbwana Samatta (KRC Genk) na Thomas Ulimwengu (JS Saoura).

Wengine ni John Bocco (Simba), Farid Mussa (Teneriffe), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kassim Hamis ( Kagera Sugar), Miraj Athuman (Lipuli), Kelvin John (Serengeti Boys) na Adi Yusuph (Solihull Moors).