Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jeremiah arudi upya, kazi bado kwa Prisons

Jeremiah arudi upya, kazi bado kwa Prisons

Muktasari:

  • Licha ya Jeremiah kufikisha mabao sita, lakini timu yake bado haijawa salama huku ikibakiwa na mechi nne kumaliza Ligi na kusubiri hatma yake.

Mbeya. Tangu alipofunga hat-triki Novemba 27, hatimaye leo Jeremiah Juma amefufuka tena akitupia bao akiisaidia Prisons kupata sare ya 1-1 dhidi ya Geita Gold.

Hata hivyo matokeo hayo yameendelea kuwaweka kwenye presha Prisons katika vita ya kushuka daraja kwani wamefikisha pointi 25 na kupanda nafasi ya 14 akiwashusha Biashara United ambao bado wana faida ya mchezo mmoja huku Mbeya Kwanza wakirudi mkiani.

Dakika 45 zilianza kwa kasi hasa wenyeji kuonesha nia ya kupata bao la mapema kutokana na mashambulizi waliyoyafanya japokuwa nafasi kadhaa walizopata hawakuweza kuzitumia vyema.

Geita Gold waliokuwa wakimtegemea kinara wake wa mabao, George Mpole, alikumbana na ulinzi mzito ambao haukumpa nafuu kupumua kupenyeza hatari zake langoni mwa Wajelajela.

Prisons waliolazimisha mashambulizi ambayo yaliweza kuwapa faida baada ya Juma kuipatia bao la kuongoza dakika ya 35 alipotumia mpira wa faulo uliopigwa na Ibrahim Abraham na kudumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Geita Gold iliingia na mabadiliko kwa kuwatoa Maka Edward na Amos Kadikilo na nafasi zao kujazwa na Ofen Chikola na Edmund John dakika ya 46, huku Prisons ikiwapumzisha Lambart Sabiyanka na Dotto Shaban na kuwaingiza Mohamed Mkopi na Omary Omary dakika ya 47.

Dakika ya 48, Geita Gold walisawazisha bao hilo kupitia kwa Daniel Lyanga baada ya Kipa wa Prisons, Hussein Abel kutoka langoni bila mawasiliano na beki wake Nurdin Chona na kumkuta mfungaji huyo aliyeuingiza wavuni.

Prisons ilifanya mabadiliko tena kwa kuwatoa Mudathir Abdullah na kuingia Benjamin Asukile huku wapinzani wakimtoa Jofrey Manyasi na kuingia Chilo Mkama katika dakika ya 80 na 83.

Prisons walipambana kusaka bao la ushindi lakini walikutana na wakati mgumu kwa wapinzani ambao nao walihitaji ushindi ili kukaa nafasi tatu za juu lakini timu zote ziliweza kutoshana nguvu kwa sare hiyo na sasa Geita Gold wanaendelea kubaki nafasi yao ya tano kwa alama 36.