Mshambuliaji Robert Lewandowski amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza katika Fainali za Kombe la Dunia na kuiwezesha Poland kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Saudi Arabia.
Mshambuliaji huyo alitoa pasi ya bao la kwanza akifunga Piotr Zielinski, baada ya ushindi huo Poland imepanda kileleni mwa msimamo wa kundi C kwa pointi nne ikifuatiwa na Saudi Arabia yenye tatu.
Lewandowski amefikia idadi sawa na Pele katikan ngazi ya timu ya taifa wote wakiwa na 77.