KIPANGA ya visiwani hapa imekuwa timu ya kwanza ya Tanzania kusonga mbele kwenye michuano ya CAF, baada ya kuingoa Al Hilal Wau ya Sudan Kusini kwa mikwaju ya penalti 4-3 na kuifuata Azam FC ilipangwa kuanzia raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa matokeo hayo Kipanga iliyorejea kwenye michuano ya CAF kwa mara ya kwanza tangu iliposhiriki mara ya mwisho mwaka 2005, itakutana na Club Africain ya Tunisia.
Hii ni mara ya pili kwa timu ya Zanzibar kufuzu raundi ya kwanza tangu 2019, Malindi ilipoing'oa Mogadishu City ya Somalia.