Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZILIPIGWA: Mapambano 10 bora zaidi ya ngumi duniani muda wote

NGUMI Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, mapambano mengi makali na ya kuvutia yaliyohusisha mabondia wakubwa yamebaki kwenye kumbukumbu za historia. Hebu kumbuka masumbwi haya ya kihistoria yalivyokuwa na kusababisha msisimko mkubwa wakati huo.

LONDON, ENGLAND: JANGA la Uviko-19 liliyafanya mambo mengi katika maisha ya binadamu kusimama. Miongoni mwa hayo mapambano mengi ya ngumi ambayo mashabiki walikuwa wakiyasubiri kwa hamu yaliahirishwa.

Hata hivyo, mapambano mengi makali na ya kuvutia yaliyohusisha mabondia wakubwa yamebaki kwenye kumbukumbu za historia. Hebu kumbuka masumbwi haya ya kihistoria yalivyokuwa na kusababisha msisimko mkubwa wakati huo.


NGUM 06

1. Muhammad Ali vGeorge Foreman, KINSHASA - ZAIRE (DRC)

Pambano hilo maarufu kama ‘Rumble in the Jungle’ lililopigwa Oktoba 30, 1974, linachukuliwa kuwa mojawapo wa mapambano ya kusisimua zaidi katika historia ya ngumi. Ulimwengu wa sasa wa ngumi unalielezea kama ushindi mkubwa wa Muhammad Ali, lakini 1974 matarajio ya bondia huyo yalionekana kuwa madogo. George Foreman alikuwa kileleni mwa uwezo wake akijulikana kwa ngumi zake nzito zilizofahamika ‘za mizinga.’

Lakini, kilichotokea ulingoni kiliwashangaza mashabiki na wachambuzi wengi wa mchezo huo. Foreman alianza pambano kwa kasi kama kawaida akitarajia kumchosha mpinzani wake. Lakini, Ali alifanikiwa kumudu janja hiyo vyema na katika raundi ya nane akampiga Foreman mfululizo kwa ngumi kali zilizomfanya ashinde kwa knockout.


NGUM 01

2. Muhammad Ali v Joe Frazier, Manila - Ufilipino

Hili lilikuwa pambano la tatu na la mwisho katika upinzani mkali kati ya mabondia wawili bora zaidi wa uzani wa juu wakati huo ambalo lilipigwa Oktoba 1, 1975.

Mabondia wote walikuwa wameshinda pambano moja kila mmoja. Hivyo pambano hili lililojulikana kama “Thrilla in Manila† lilikuwa la kuamua nani bora.

Pambano hilo lilidumu kwa raundi 14, likiwaacha wote wawili wakiwa wamechoka vibaya. Frazier alipata maumivu mengi na hatimaye pambano likasimamishwa kwa uamuzi wa timu yake. Ali alitangazwa mshindi, lakini timu yake ilisema kuwa kama Frazier asingesalimu amri wao pia wangeamua kulisimamisha.

Baada ya pambano, Ali alimuomba Frazier msamaha kwa maneno ya dharau aliyomsema kabla ya pambano, na baadaye akawa akizungumza juu yake kwa heshima kubwa. Hata hivyo, Frazier alijitenga na Ali baada ya pambano hilo.


NGUM 02

3. Marvin Hagler v Thomas Hearns, Las Vegas-Marekani

Katika miaka ya 1980, kila pambano lililomhusisha Sugar Ray Leonard, Roberto Duran, Marvin Hagler na Thomas Hearns lilikuwa tukio kubwa. Wanne hawa walikuwa wakipigana kuthibitisha nani bora zaidi.

Hagler na Hearns walikutana mara moja tu ulingoni, lakini pambano hilo lililoitwa ‘Vita’ liliingia kwenye historia kama mojawapo ya mapambano yenye burudani zaidi kuwahi kutokea na hadi leo linachukuliwa kama kielelezo cha ubora wa ngumi. Ngumi zilipigwa Aprili 4, 1985.


NGUM 03

4. Sugar Ray Leonard v Marvin Hagler, Las Vegas - Marekani

Pambano hilo lililopigwa Aprili 4, 1985 linaelezwa kuwa moja ya mapambano yenye msisimko mkubwa yasiyotegemewa na yenye matokeo ya kushangaza. Kabla ya pambano, Hagler ambaye alikuwa bingwa wa dunia wa uzani wa light middleweight alionekana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda.

Sugar Ray Leonard alikuwa hajapigana kwa miaka mitatu, lakini kuanzia raundi ya kwanza alionyesha ubora wake wa zamani. Alitawala pambano zima na baada ya Hagler kupoteza alishindwa kuvumilia mshtuko huo na akaamua kustaafu.


NGUM 04

5. Roberto Duran v vIran Barkley, Las Vegas-Marekani

Roberto Duran alikuwa bondia mwenye historia tata na ya kuvutia. Katika uzani wa light-heavyweight alikuwa bora. Lakini alipohamia katika uzani wa juu zaidi bahati ilianza kumpa kisogo.

Februari 24, 1989, Duran akiwa mzee na mashabiki wengi hawakumtegemea kushinda pambano dhidi ya Iran Barkley ambaye alikuwa amemshinda Thomas Hearns kwenye pambano lililotangulia, lakini alishangaza wengi kwani alimudu raundi zote 12 kwa ubora mkubwa na kushinda kwa uamuzi wa majaji.


NGUM 05

6. Marco Antonio Barrera v Erik Morales, Las Vegas-Marekani

Hawa ni mabondia wawili wa Mexico waliokuwa na uhasama binafsi wa muda mrefu. Kila walipokutana ulingoni ilikuwa kama kuzimu. Walipigana mara tatu, lakini pambano lao la kwanza ndilo lilikuwa kali zaidi na lenye kuvutia zaidi na likabaki kuwa moja ya mapambano bora likipigwa Februari 19, 2000.


NGUM 07

7. Israel Vazquez v Rafael Marquez, Carson - Marekani

Mabondia hawa walipigana mara nne kila mmoja akishinda mara mbili. Pambano lao la tatu lililopigwa Machi 1, 2008 ndilo lililovutia zaidi likichukuliwa kuwa mojawapo ya mapambano mazuri zaidi kati ya Wamexico wawili kwenye historia ya ngumi.


NGUM 08

8. Arturo Gatti v Micky Ward, Ancasville - Marekani

Wamepigana mara tatu kila pambano likiwa gumu na lenye kuvutia. Wachambuzi wa masumbwi walitofautiana kuhusu lipi bora zaidi, lakini wengi walikubaliana kuwa pambano la kwanza lililopigwa Mei 18, 2002 aliloshinda Ward ndilo lilikuwa la kuvutia zaidi. Mwishowe, Gatti alishinda jumla ya mapambano 2-1.


NGUM 09

9. Mike Tyson v Evander Holyfield, Las Vegas, Marekani

Wachambuzi wa ngumi wengi duniani wanaliita hili pambano bora zaidi la muongo wa mwisho wa karne ya 20. Lilitangazwa mara ya kwanza 1991, lakini likaahirishwa mara kadhaa hadi Juni 28, 1997. Wakati huo, mabondia hao wote walikuwa wamefikia kilele cha uwezo wao. Hata hivyo, mashabiki walilipwa deni wakishuhudia raundi 11 za ngumi za kiwango cha juu. Tyson alipoteza kwa knockout, lakini pambano hilo lilibaki kwa miaka 21 likichukuliwa kama bora zaidi la uzani wa juu dunia.


NGUM 10

10. Anthony Joshua v Wladimir Klitschko, London- Uingereza

Wakati pambano hili lilipotangazwa mashabiki wengi wa ngumi duniani walimpa ushindi Anthony Joshua, kijana mwenye nguvu na mafanikio makubwa. Wladimir Klitschko akiwa na umri wa miaka 41, alikuwa amepita kipindi chake cha utawala. Pambano hilo lililopigwa Aprili 29, 2017 lilidumu kwa raundi 11 na Joshua akashinda kwa TKO. Hata hivyo, haikuwa kazi rahisi kwani Klitschko alionyesha ubora wa hali ya juu na kuhitimisha taaluma yake kwa heshima.

Ukiachana na mapambano hayo 10 bora, lakini kuna kitu kama bonasi kwa mashabiki wa ngumi na wachambuzi wa mchezo huo duniani kutokana na pambano kati ya Ricardo Torres dhidi ya Kendall Holt likiwa ni la pili kati yao ambalo lilipigwa Julai 5, 2008, huko Las Vegas, Marekani.

Hilo lilikuwa pambano la kulipiza kisasi kwa Kendall Holt baada ya Torres kumshinda kwa knockout mwaka uliotangulia. Safari hii Holt alitumia nafasi yake vyema  akimshinda Torres kwa knockout ndani ya dakika moja tu ya raundi ya kwanza.

Pambano hilo linajulikana kama mojawapo ya mapambano mafupi zaidi kati ya mabondia wa viwango sawa. Pambano lingine katika bonasi ya mashabiki na wachambuzi wa ngumi wanalolitaja duniani ni lile la Floyd Mayweather na Manny Pacquiao lililopigwa Mei 2, 2015 huko Las Vegas, Marekani.

Kabla ya pambano hilo Mayeweather alikuwa na rekodi ya kupigana mara 47 bila kupoteza huku akishinda mara 26 kwa knockout ilhali Pac-man alikuwa amepigana mapambano 57, sare tano na vipigo viwili, lakini akiwalambisha mchanga wapinzani wake mara 38 kwa knockout.

Hadi leo, pambano kati ya wawili hao linashikilia rekodi ya mauzo ya runinga Marekani upande wa pay-per-view (PPV) yaani malipo ya kutazama tukio kwa mashabiki wanaokuwa majumbani, likifikia milioni 4.6 kupitia televisheni maarufu za michezo HBO na Showtime.

Pambano hilo lililoitwa ‘Fight of the Century’ lilikuwa na mafanikio makubwa kiasi cha kuingiza mapato ya Dola 600 milioni pamoja na malipo ya PPV kwani watu walilipia kati ya Dola 90 hadi 100 kwa HD kuwaangalia tu wababe hao wakizichapa.