Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WATATOBOA, HAWATOBOI: Kila mmoja ana msala wake Ligi Kuu England

KUTOBOA Pict

Muktasari:

  • Timu tatu za mkiani Southampton, Leicester na Ipswich Town nazo zinaonekana kama ndizo ambacho zitang'oka kwenye ligi hiyo na kushuka daraja msimu huu.

LONDON, ENGLAND: MSIMU wa Ligi Kuu England unaelekea ukingoni huku Liverpool ikijiweka kwenye wakati mzuri wa kunyakua taji lao la pili la michuano hiyo.

Timu tatu za mkiani Southampton, Leicester na Ipswich Town nazo zinaonekana kama ndizo ambacho zitang'oka kwenye ligi hiyo na kushuka daraja msimu huu.

Lakini, kuna timu nyingine zipo kwenye vita kali ya kuwania tiketi za kucheza michuano ya Ulaya kwa msimu ujao.

Kutokana na nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kutoa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao - msako wa tiketi za kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao, inaweza kuhusisha hadi timu inayoshika namba 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Kutokana na hilo, vita ya kusaka tiketi ya michuano ya Ulaya imenoga balaa.

Hata hivyo, kwa vita zote zinazoshindaniwa kwa msimu huu, kuanzia kwenye mchakamchaka wa ubingwa, ambapo Arsenal inajaribu kuifukuzia Liverpool, kwenye Top Four, ambapo mabingwa watetezi Manchester City wanajaribu kujipenyeza kwenye eneo hilo na ile ya kupambana kubaki kwenye ligi, kinachoangaliwa ni timu gani imebakiza mechi ngumu katika kuelekea mwisho wa msimu huu?

Crystal Palace na Newcastle United pekee ndizo zilizobakiza mechi 10, lakini nyingine zote zilizobaki zimebakiza mechi tisa kabla ya msimu huu kufika tamati. Timu gani ina ratiba yenye kuhitaji ujanja mwingi kutoboa? Twende kazi.


KUT 01

1. Liverpool - mechi 29, pointi 70

Liverpool imejiweka kwenye nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, ikiongoza msimamo kwa tofauti ya pointi 12 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo, Arsenal na bado kuna mechi tisa za kucheza. Kutokana na hilo, Liverpool imejiweka pazuri kubeba taji lake la pili la Ligi Kuu England msimu huu.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Everton (nyumbani)

Aprili 6 - Fulham (ugenini)

Aprili 13 - West Ham (nyumbani)

Aprili 20 - Leicester (ugenini)

Aprili 27 - Tottenham (nyumbani)

Mei 3 - Chelsea (ugenini)

Mei 10 - Arsenal (nyumbani)

Mei 18 - Brighton (ugenini)

Mei 25 - Crystal Palace (nyumbani)


KUT 02

2. Arsenal - mechi 29, pointi 58

Inavyoonekana, Arsenal inakwenda kumaliza nafasi ya pili tena kwa msimu wa tatu mfululizo kwenye Ligi Kuu England, baada ya sasa kuachwa nyuma pointi 12 na vinara Liverpool, huku kila timu ikiwa na mechi tisa za kucheza. Ilipo Arsenal imejiweka pazuri kwenye kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku ikifukuzia ubingwa kisirisiri.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 1 - Fulham (nyumbani)

Aprili 5 - Everton (ugenini)

Aprili 12 - Brentford (nyumbani)

Aprili 20 - Ipswich (ugenini)

Aprili 26 - Crystal Palace (nyumbani)

Mei 3 - Bournemouth (nyumbani)

Mei 10 - Liverpool (ugenini)

Mei 18 - Newcastle (nyumbani)

Mei 25 - Southampton (ugenini)


KUT 03
KUT 03

3. Nottingham Forest - mechi 29, pointi 54

Ikirejea kwenye makali yake ya zamanbi, Nottingham Forest kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, pointi nne tu nyuma ya Arsenal iliyopo kwenye nafasi ya pili katika msimamo huo, lakini ikiwa pointi tano juu ya Chelsea inayokamilisha Top Four. Kupata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Forest inahitaji kushikilia iliposhika hadi mwisho.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 1 - Man United (nyumbani)

Aprili 5 - Aston Villa (ugenini)

Aprili 12 - Everton (nyumbani)

Aprili 21 - Tottenham (ugenini)

Aprili 26 - Brentford (nyumbani)

Mei 3 - Crystal Palace (ugenini)

Mei 10 - Leicester (nyumbani)

Mei 18 - West Ham (ugenini)

Mei 25 - Chelsea (nyumbani)


KUT 04

4. Chelsea - mechi 29, pointi 49

Ikiwa kwenye nafasi ya nne kwa sasa, Chelsea inaamini itabaki kwenye eneo hilo na kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya ushindani wa jambo hilo unalihusu timu inayoshika namba nne hadi 10 kwenye msimamo huo. Kinachotia wasiwasi ni mwenendo wao kwamba unaweza kuwagharimu kupata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 3 - Tottenham (nyumbani)

Aprili 6 - Brentford (ugenini)

Aprili 13 - Ipswich (nyumbani)

Aprili 20 - Fulham (ugenini)

Aprili 26 - Everton (ugenini)

Mei 3 - Liverpool (nyumbani)

Mei 10 - Newcastle (ugenini)

Mei 18 - Man United (nyumbani)

Mei 25 - Nottm Forest (ugenini)


KUT 05

5. Man City - mechi 29, pointi 48

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Manchester City kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo, pointi moja nyuma ya Chelsea iliyopo kwenye namba nne, lakini ipo pointi nne tu juu ya timu inayoshika nafasi ya 10 kwenye msimamo, jambo linaloonyesha jinsi timu zilivyoachana kwa pointi chache. Man City inahitaji kuchanga vyema karata zake.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Leicester (nyumbani)

Aprili 6 - Man United (ugenini)

Aprili 12 - Crystal Palace (nyumbani)

Aprili 19 - Everton (ugenini)

Aprili 28 - Aston Villa (nyumbeni)

Mei 3 - Wolves (nyumbani)

Mei 10 - Southampton (ugenini)

Mei 18 - Bournemouth (nyumbani)

Mei 25 - Fulham (ugenini)


KUT 06

6. Newcastle - mechi 28, pointi 47

Imetoka kunyakua taji la Kombe la Ligi, ikimaliza ukame wa mataji wa miaka 70, Newcastle United ipo nyuma pointi moja tu kuingia kundi la timu zitakazoshinda tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, hivyo inahitaji kukamatia hapohapo kutoka sasa hadi mwisho wa msimu kuhakikisha inavuna pointi za kucheza michuano ya Ulaya.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Brentford (nyumbani)

Aprili 7 - Leicester (ugenini)

Aprili 13 - Man United (nyumbani)

Aprili 16 - Crystal Palace (nyumbani)

Aprili 19 - Aston Villa (ugenini)

Aprili 26 - Ipswich (nyumbani)

Mei 3 - Brighton (ugenini)

Mei 10 - Chelsea (nyumbani)

Mei 18 - Arsenal (ugenini)

Mei 25 - Everton (nyumbani)


KUT 07

7. Brighton - mechi 29, pointi 47

Pointi moja tu nyuma ya nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, Brighton inaamini inaweza kufanya jambo kutokana na kutokuwa na ratiba inayotisha sana kwenye mechi zake zilizobaki kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Hata ikikosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, Seagulls itataka kucheza Ulaya msimu ujao.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Aston Villa (nyumbani)

Aprili 5 - Crystal Palace (ugenini)

Aprili 12 - Leicester (nyumbani)

Aprili 19 - Brentford (ugenini)

Aprili 26 - West Ham (nyumbani)

Mei 3 - Newcastle (nyumbani)

Mei 10 - Wolves (ugenini)

Mei 18 - Liverpool (nyumbani)

Mei 25 - Tottenham (ugenini)


KUT 08

8. Fulham - mechi 29, pointi 45

Kwa sasa inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi, Fulham inaamini itafanya mapinduzi kwenye mechi za mwisho na kunyakua tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kutokana na sasa kuwa nyuma kwa pointi tatu tu dhidi ya Man City waliopo kwenye nafasi ya tano. Lakini, ratiba yao ya mechi zilizobaki ni ngumu sana, itatoboa?


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 1 - Arsenal (ugenini)

Aprili 6 - Liverpool (nyumbani)

Aprili 14 - Bournemouth (ugenini)

Aprili 20 - Chelsea (nyumbani)

Aprili 26 - Southampton (ugenini)

Mei 3 - Aston Villa (ugenini)

Mei 10 - Everton (nyumbani)

Mei 18 - Brentford (ugenini)

Mei 25 - Man City (nyumbani)


KUT 09

9. Aston Villa - mechi 29, pointi 45

Aston Villa imeketi pointi tatu nyuma ya Man City kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, huku ikiwa na msimu mtamu kabisa baada ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na itakipiga na Paris Saint-Germain. Mwenendo wa Aston Villa si mbaya na kama itachanga vyema karata zake, itacheza tena Mabingwa Ulaya msimu ujao.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Brighton (ugenini)

Aprili 5 - Nottm Forest (nyumbani)

Aprili 12 - Southampton (ugenini)

Aprili 19 - Newcastle (nyumbani)

Aprili 28 - Man City (ugenini)

Mei 3 - Fulham (nyumbani)

Mei 10 - Bournemouth (ugenini)

Mei 18 - Tottenham (nyumbani)

Mei 25 - Man United (ugenini)


KUT 10

10. Bournemouth - mechi 29, pointi 44

Kwenye nafasi ya 10 katika msimamo, lakini ipo nyuma pointi nne tu dhidi ya Man City iliyopo kwenye nafasi ya tano, ambayo inayotoa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Bournemouth imekuwa na kiwango kizuri msimu huu na kuchuana kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya kwa msimu ujao. Ikipambana, itafanikiwa.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Ipswich (nyumbani)

Aprili 5 - West Ham (ugenini)

Aprili 14 - Fulham (nyumbani)

Aprili 19 - Crystal Palace (ugenini)

Aprili 27 - Man United (nyumbani)

Mei 3 - Arsenal (ugenini)

Mei 10 - Aston Villa (nyumbani)

Mei 18 - Man City (ugenini)

Mei 25 - Leicester (nyumbani)


KUT 11

11. Brentford - mechi 29, pointi 41

Ipo kwenye nafasi ya 11, lakini pointi saba tu nyuma ya nafasi za kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, hivyo miamba hiyo bado haijakata tamaa kwenye msako wao wa tiketi hiyo. Lakini, kinachoonekana upande wao, nafasi kubwa ni kushinda tiketi ya kucheza mikikimikiki ya Conference League msimu ujao kutokana na ratiba yao kuhitaji ujanja sana.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Newcastle (ugenini)

Aprili 6 - Chelsea (nyumbani)

Aprili 12 - Arsenal (ugenini)

Aprili 19 - Brighton (nyumbani)

Aprili 26 - Nottm Forest (ugenini)

Mei 3 - Man United (nyumbani)

Mei 10 - Ipswich (ugenini)

Mei 18 - Fulham (nyumbani)

Mei 25 - Wolves (ugenini)


KUT 12
KUT 12

12. Crystal Palace - mechi 28, pointi 39

Nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi, lakini haionekani kama Crystal Palace itakuwa na nafasi ya kukamatia tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya. Kwenye nafasi hiyo Palace inaonekana kuwa kwenye nafasi itakayowafanya wabaki kwenye ligi msimu ujao licha ya mzunguko wa pili kwa ligi kuwa na matokeo magumu kwao, inahitaji kupambana.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Southampton (ugenini)

Aprili 5 - Brighton (nyumbani)

Aprili 12 - Man City (ugenini)

Aprili 16 - Newcastle (ugenini)

Aprili 19 - Bournemouth (nyumbani)

Aprili 26 - Arsenal (ugenini)

Mei 3 - Nottm Forest (nyumbani)

Mei 10 - Tottenham (ugenini)

Mei 18 - Wolves (nyumbani)

Mei 25 - Liverpool (ugenini)


KUT 13

13. Man United - mechi 29, pointi 37

Chini kwenye nafasi ya 13 baada ya kuwa na msimu wa hovyo, Manchester United haionekani kabisa kama itacheza michuano ya Ulaya kupitia ligi ya ndani ya msimu ujao, labda kama tu itafanya maajabu kwenye mechi zilizobaki na kupindua meza. Lakini, rayiba yao ilivyo, imeonekana kuwa ngumu kwenye kulitimiza hilo na kuwa na vita kali ya kupigana.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 1 - Nottm Forest (ugenini)

Aprili 6 - Man City (nyumbani)

Aprili 13 - Newcastle (ugenini)

Aprili 20 - Wolves (nyumbani)

Aprili 27 - Bournemouth (ugenini)

Mei 3 - Brentford (ugenini)

Mei 10 - West Ham (nyumbani)

Mei 18 - Chelsea (ugenini)

Mei 25 - Aston Villa (nyumbani)


KUT 14

14. Tottenham - mechi 29, pointi 34

Msimu umekuwa mbaya sana kwa Tottenham Hotspur, ikishika nafasi ya 14 katika msimamo huo. Haipo kwenye hatari ya kushuka daraja, lakini ipo mbali sana na pointi za kukamatia tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao. Kiwango chao kibovu kimeanza kumfanya kocha kuwa kwenye hatari ya kupoteza ajira yake kama hali haitabadilika.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 3 - Chelsea (ugenini)

Aprili 6 - Southampton (nyumbani)

Aprili 13 - Wolves (ugenini)

Aprili 21 - Nottm Forest (nyumbani)

Aprili 27 - Liverpool (ugenini)

Mei 3 - West Ham (ugenini)

Mei 10 - Crystal Palace (nyumbani)

Mei 18 - Aston Villa (ugenini)

Mei 25 - Brighton (nyumbani)


KUT 15

15. Everton - mechi 29, pointi 34

Mambo yalionekana kuwa mabaya kiasi cha kutishia kwamba Everton ingeshuka daraja msimu huu hadi hapo kocha David Moyes alipokuja na kubadili hali ya mambo na kuiweka timu hiyo kwenye nafasi ya kuendelea kubaki kwenye ligi. Everton ilikutana na mechi ngumu na zote ilizocheza vizuri kama ambavyo inaaminika itazicheza zilizobaki kumaliza msimu.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Liverpool (ugenini)

Aprili 5 - Arsenal (nyumbani)

Aprili 12 - Nottm Forest (ugenini)

Aprili 19 - Man City (nyumbani)

Aprili 26 - Chelsea (ugenini)

Mei 3 - Ipswich (nyumbani)

Mei 10 - Fulham (ugenini)

Mei 18 - Southampton (nyumbani)

Mei 25 - Newcastle (ugenini)


KUT 16

16. West Ham - mechi 29, pointi 34

Nafasi ya 16 kwenye msimamo wa ligi, pointi 17 juu ya shimo la kushuka daraja, lakini pointi nyingi kuifikia tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya, West Ham United inahitaji kufanya maajabu makubwa kwenye mechi zake zilizobaki ili kukamatia tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya baada ya kuonekana kama ishu ya kubaki kwenye ligi ni kubwa.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 1 - Wolves (ugenini)

Aprili 5 - Bournemouth (nyumbani)

Aprili 13 - Liverpool (ugenini)

Aprili 19 - Southampton (nyumbani)

Aprili 26 - Brighton (ugenini)

Mei 3 - Tottenham (nyumbani)

Mei 10 - Man United (ugenini)

Mei 18 - Nottm Forest (nyumbani)

Mei 25 - Ipswich (ugenini)


KUT 17

17. Wolves - mechi 29, pointi 26

Kwenye nafasi ya 17 katika msimamo wa Ligi Kuu England na pointi nane nyuma ya West Ham iliyopo kwenye namba 16 katika msimamo huo, Wolves itahitaji kushinda mechi zake zilizobaki ili isijikute kwenye shimo la kushika daraja. Kwa sasa ipo pointi tisa juu ya Ipswich iliyopo kwenye nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi hiyo. Inapaswa kujipanga.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 1 - West Ham (nyumbani)

Aprili 5 - Ipswich (ugenini)

Aprili 13 - Tottenham (nyumbani)

Aprili 20 - Man United (ugenini)

Aprili 26 - Leicester (nyumbani)

Mei 3 - Man City (ugenini)

Mei 10 - Brighton (nyumbani)

Mei 18 - Crystal Palace (ugenini)

Mei 25 - Brentford (nyumbani)


KUT 18

18. Ipswich - mechi 29, pointi 17

Pointi tisa nyuma ya timu inayoshika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, Wolves, Ipswich Town imekuwa kivutio kwa wengi kutokana na staili yao ya uchezaji, lakini matokeo yamekuwa magumu kwao na kujiweka kwenye hatari kubwa ya kushuka daraja na kurejea kwenye Championship. Inahitaji kubadilika ili kubaki kwenye ligi.


MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Bournemouth (nyumbani)

Aprili 5 - Wolves (nyumbani)

Aprili 13 - Chelsea (ugenini)

Aprili 20 - Arsenal (nyumbani)

Aprili 26 - Newcastle (ugenini)

Mei 3 - Everton (ugenini)

Mei 10 - Brentford (nyumbani)

Mei 18 - Leicester (ugenini)

Mei 25 - West Ham (nyumbani)


KUT 19

19. Leicester - mechi 29, pointi 17

Inalingana pointi na Ipswich, lakini Leicester City ipo kwenye nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi na kama itashindwa kufanya mabadiliko ya matokeo yao basi msimu ujao utawahusu kucheza kwenye Championship. Ratiba yao ya mechi zilizobaki zinahitaji ujanja mwingi sana kushinda na hicho ndicho kinachowaweka kwenye wakati mgumu miamba hiyo ya King Power.

MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Man City (ugenini)

Aprili 7 - Newcastle (nyumbani)

Aprili 12 - Brighton (ugenini)

Aprili 20 - Liverpool (nyumbani)

Aprili 26 - Wolves (ugenini)

Mei 3 - Southampton (nyumbani)

Mei 10 - Nottm Forest (ugenini)

Mei 18 - Ipswich (nyumbani)

Mei 25 - Bournemouth (ugenini)


KUT 20

20. Southampton - mechi 29, pointi 9

Moja ya timu zilizofanya vibaya zaidi kwenye Ligi Kuu England msimu huu ni Southampton, ambapo imevuna pointi tisa tu kati ya 87 na kwa hali ilivyo, hakuna kinachoonekana kitainusuru timu hiyo kushuka daraja msimu huu. Kinachoonekana kwa sasa ni kwamba Southampton inakabilisha tu ratiba kwenye Ligi Kuu England ili ikacheze Championship.

MECHI ZILIZOBAKI;

Aprili 2 - Crystal Palace (nyumbani)

Aprili 6 - Tottenham (ugenini)

Aprili 12 - Aston Villa (nyumbani)

Aprili 19 - West Ham (ugenini)

Aprili 26 - Fulham (nyumbani)

Mei 3 - Leicester (ugenini)

Mei 10 - Man City (nyumbani)

Mei 18 - Everton (ugenini)

Mei 25 - Arsenal (nyumbani)